February 2, 2018

RAIS JPM AMTUMBUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI USIKU

                                

Rais wa Tanzania John Magufuli                    Rais wa Tanzania John Magufuli                
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dokta Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali.
Uteuzi huo umeanza jana, Februari mosi.
Kabla ya uteuzi huo Dokta Kilangi, alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughili za mkondo wa juu ya mafuta-PURA.
Wakati huohuo, Rais Magufuli amemteua Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali.
Kabla ya uteuzi huo alikuwa Paul Ngwembe, Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania.

Kufuatia uteuzi huo, Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali George Mcheche Masaju na Aliyekuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama kuu.
Uteuzi huo pia umeanza jana Februari mosi

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE