February 9, 2018

PIKIPIKI ZILIZOKAMATWA NA POLISI YA TANZANIA KUACHIWA


PIK1 WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba akikagua pikipiki ambazo zimeshikiliwakatika kituo cha polisi pangani. ameagiza polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.
………………………………………………………………………………….
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.
Dk Mwigulu amesema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya, na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazitatua haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.
“Wapeni masomo wamekosea wapi walekezeni na waliowabishi waelekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunawo, tutumie huu mkono wakutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” alisema Dk Mwigulu
Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila napopita kita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.
PIK2

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE