February 22, 2018

Pakistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Afghanistan ni nchi hatari zaidi kuzaliwa mtoto

 Pakistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Afghanistan ni nchi hatari zaidi kuzaliwa mtoto
Idadi kubwa ya watoto wanapoteza maisha punde wanapozaliwa katika maeneo ya kati na magharibi mwa Afrika licha ya kuwa afya ya mtoto imeboreka kiujumla duniani, imesema Idara ya Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Watoto, UNICEF.

Ripoti hiyo imebaini kuwa, watoto wanaozaliwa katika maeneo ya kati na magharibi mwa Afrika wanakabliwa na janga la mauti mwezi moja baada ya kuzaliwa.

Ripoti hiyo imetaja nchi ambazo ni bora zaidi kuzaliwa watoto ambazo ni pamoja na Japan, Iceland na Singapore huku watoto wanaozaliwa Pakistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Afghanistan wakiwa katika hatari zaidi ya kufariki dunia.

Aidha UNICEF imesema kuwa, nchi 8 kati ya 10 ambako ni hatari zaidi kuzaliwa ziko barani Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.

Sababu za vifo ni pamoja na kuzaliwa njiti, matatizo ya wakati wa kujifungua na maambukizi ya magonjwa kama vile vichomi.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Henrietta H. Fore amesema ingawa takwimu zinaonyesha kuwa robo karne iliyopita idadi ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ilipungua kwa asilimia 50, bado  kuna tatizo kwa watoto wenye umri wa chini ya mwezi mmoja.

Kwa kutambua hilo, mwezi huu UNICEF inazindua kampeni mahsusi iiliyopewa jina la  Kila Mtoto Awe Hai au Every Child ALIVE.

UNICEF kupitia kampeni hiyo inazitaka serikali, wahudumu wa afya, wahisani, sekta binafsi na familia zichukue hatua kuhakikisha huduma za afya zinapatikana ili kulinda uhai wa watoto hao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE