February 22, 2018

NAIBU WAZIRI AWESO -WAKANDARASI WASIO WAZALENDO WASIPEWE KAZI NDANI YA JIJI LA DAR

 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na mmoja ya wafanyakazi wa ujenzi wa mradi huo. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG- DAR. Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amewataka wakandarasi walio wazembe wasipewe kazi kwa  vile wamekuwa wakirudisha nyuma maendeleo kwa kuwakosesha wananchi kupata maji kwa wakati.

 Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara katika wilaya ya Kinondoni ili kujionea ujenzi mbali mbali ya miundo mbinu inayoendeshwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na Shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO). 

Naibu Waziri Aweso amesema kuwa wakati umefika kwa wale wakandarasi wazembe kuacha kuchezea kazi wanazopewa, wafanye kazi kwa bidii ili huduma za maji zitolewe kwa wakati. 

 "Nawaomba sana wale wakandarasi wazembe waache kuwepewa kazi maana wanachafua wilaya ya Kinondoni na Tanzania kwa ujumla maana nimetembelea miradi mbali mbali nimejionea uzembe unaofanywa na wakandarasi, ukiangalia mkandarasi kapewa hela asilimia 70 ila kazi aliyofanya ya asilimia 40 hii haikubaliki kabisa. 

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amemshukuru Naibu Waziri Aweso kwa msikamano ambao amekuwa akiufanya na wilaya yake ya kuwapa kipaumbele cha kuwatembelea mara kwa mara hali inayoamsha maendeleo zaidi. 

 "Mimi sina mengi nitatekeleza maelekezo yote ambayo ameyatoa na nitakuwa msitari wa mbele kutoa maamuzi ya kina kwa wale makandarasi wazembe, sitamuonea aibu mtu,' amesema Naibu Waziri Aweso. 

 Nae Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASCO, Injinia Aron Joseph amewaomba wananchi kuendelea kuwa wavumilivu kwa vile kwasasa wamejipanga zaidi kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa walio pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.

 "Tunamalizia ujenzi wa matanki makubwa ambayo tutaweza kuwasambazia wananchi wengi zaidi maji hasa walioko pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam," amesema Injinia Aron.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE