February 15, 2018

MWANDISHI IRINGA AKAMATWA NA POLISI AKIWA KATIKA MAJUKUMU YAKE


Mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa, Geofrey Nyang'oro amekamatwa na polisi.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), Frank Leonard ameiambia Matukiodaima  kuwa mwandishi huyo wa habari amekamatwa na polisi wakati akiwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa leo Alhamis Februari 15,2018.

Amesema wanaendelea kufuatilia sababu za kukamatwa kwake .


"Ni kweli tumepata taarifa za kuwa Nyang'oro amekamatwa kwa mahojiano na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai (RCO) tunafuatilia kujua zaidi" amesema

Mwandishi huyu na wenzake walikuwa mahakamani hapo kuripoti kesi ya Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE