February 12, 2018

MWAKYEMBE AHIMIZA UTUNZAJI WA HISTORIA


mwakyembe
Na Florah Raphael.
Waziri wa sanaa, michezo na utamaduni Dkt.Harrison Mwakyembe leo ametembelea jengo ambalo lilikuwa linatumika kwa shughuli mbalimbali wakati wa kupigania Uhuru wa bara la Afrika lililoko jijini Dar es salaam ambapo Tanzania ndiyo iliyochaguliwa kuwa makao makuu ya kumbukumbu ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika.
IMG-20180212-WA0002
Akiongea na waandishi wa habari katika eneo hilo Dkt.Harrison amesema kuwa historia ya jengo hilo ambalo lipo katikati ya  jiji la Dar es salaam limejengwa hata kabla ya Tanzania kupata uhuru na kusema kuwa lilijengwa mwaka 1958 baada tu ya Ghana kupata uhuru,huku viongozi mbalimbali kutoka Afrika akiwemo Nyerere wakiunda chama chenye nguvu cha kupigania uhuru ndani ya bara la Afrika kilichojulikana kwa jina la PAN Africanism.
Pia Dkt.Harrison amesema kuwa baada ya chama hicho kuanzishwa kilisaidia nchi nyingi kupata uhuru toka mwaka 1958 ikiwepo Tanzania iliyopata uhuru mwaka 1961 na kuongeza kuwa baada ya hapo waliamua kuanzisha umoja wa nchi huru za Afrika OAU mwaka 1963 ambapo takribani nchi 32 zilikuwa wanachama kwa lengo moja tu la kuhakikisha wanaharakisha ukombozi kwa nchi zote za bara la Afrika.
Aidha amesema kuwa jengo hilo lina umuhimu mkubwa kwa historia ya Afrika na kwa vizazi vijavyo ili kuweka kumbukumbu nzuri na kuonyesha utendaji Kazi na Juhudi za wazee wa zamani katika kuleta ukombozi kwa bara la Afrika na kuwahasa Watanzania kulinda vitu ambazo vinaonekana ni kumbukumbu kwa historia yetu ya zamani.
download
Kwa upande wake mkurugenzi wa programu ya historia ya urithi wa bara la Afrika Ingiahedi C. Mduma amesema kuwa jengo hilo ni jengo la ukombozi wa Afrika na wapigania uhuru wa Afrika wametumia jengo hilo lakini baada ya nchi za Afrika kupata uhuru jengo hilo limekuwa kama linasahaurika lakini kwa sasa limefanyiwa ukarabati na kusema kuwa ukarabati wa awamu ya kwaza umegharimu milioni 200.
Pia mkurugenzi huyo ameongeza kuwa jengo bado linahitaji ukarabati na kusema kuwa serikali imetoa milioni 700 ambapo mpaka sasa Wizara ya fedha imeshatoa milioni 250 na pia wana mpango wa kununua magari mawili yatakayogharimu milioni 226.
Pia amebainisha kuwa ukarabati wa jengo hilo utakapokamilika wanategemea kukuza uchumi wa nchi kwa kuanzisha miladi mbalimbali ambayo itasaidia itatangaza urithi na utalii wa utamaduni na maonyesho ya picha mbalimbali za kumbukumbu za zamani.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE