February 12, 2018

MKURUGENZI WA MJI HALMASHAURI YA MAFINGA SAADA MWARUKA ATOA TAARIFA HII KWA MAKAMU WA RAIS


TAARIFA FUPI YA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA IHONGOLE KWA MHESHIMIWA SAMIA
SULUHU HASSAN MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAREHE 11/02/2018

1:0 Utangulizi

Mheshimiwa Makamu wa Rais;

Tunayo furaha kubwa kukukaribisha katika Halmahauri yetu. Halmashauri ya Mji Mafinga ina

jumla ya wakazi 71,641 kati yao wanaume ni 34,522 na wanawake 37,119 (Sensa ya watu na

makazi 2012). Halmashauri ina jumla ya vituo 21 vya kutolea huduma za Afya, ikiwemo

Hospitali 1, vituo vya Afya 5 (2 vya serikli na 3 visivyo vya Serikali) na zahanati 15 (9 za

serikali na 6 zisizo za Serikali).

1.1: Utoaji wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto

Lengo ni kupuguza vifo vya akina Mama, watoto wachanga na watoto wenye umri chini ya

miaka mitano kwa kuboresha afya ya uzazi. Utekelezaji wa lengo hili ni kama ifuatavyo:-

Vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja vimepungua kutoka vifo 17/1000LB mwaka 2016

hadi kufikia 13/1000LB Desemba 2017. Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua

kutoka vifo 22/1000LB mwaka 2016, hadi kufikia 15/1000LB kufikia Desemba. Kiwango cha

vifo vitokanavyo na uzazi mwaka 2016 ilikua 182/100000 ambavyo vimepungua hadi kufikia

116/100000LB Desemba 2017. Kiwango cha wanaojifungua katika vituo vya kutolea huduma

kimeongezeka kutoka asilimia 98.5 mwaka 2016 hadi kufikia 98.8% mwaka 2017.

1.2: Mapambano Dhidi Ya UKIMWI

Hali ya maambukizi ya UKIMWI bado ni changamoto kubwa kwa jamii yetu. Katika kipindi

cha mwaka 2017/2018 jumla ya watu 29,080 (wanaume 14,180 na wanawake 14,900)

walipimwa. Waliokutwa na maambukizi ni 1,864 sawa na asilimia 6.4, kati yao wanaume ni

671 na wanawake 1,193.

1.3: Jamii Kujiunga na CHF/TIKA.

Halmashauri imeendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya Afya hasa kupitia

CHF/TIKA, hadi sasa jumla ya vituo 11 vya serikali vinatoa huduma za Afya kwa kutumia kadi

za CHF/TIKA. Hadi Desemba 2017 jumla ya wananchama 10,256 wamejiunga na CHF/BIMA

sawa na asilimia 59.7 ya walengwa.

1.4: CHANGAMOTO YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KATIKA MJI WA MAFINGA

_ Hospitali ya Mji Mafinga inapokea wagonjwa wa rufaa kutoka katika vituo vya Afya na

zahanati zilizopo kwenye Halmashauri ya Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,

Pia inahudumia wagonjwa kutoka Halmashauri za Iringa vijijini, Makambako,

Kilombelo, Mbalali, wasafiri na majeruhi wanaotumia barabara ya Dar es salaam-

Mbeya. Kiasi cha fedha kinachotengwa na Serikali kwenye Hospitali ya Mafinga

kinaangalia kigezo cha idadi ya wakazi ambao ni 71,641 wakati inahudumia wakazi

317,731 ambao ni Zaidi ya wakazi wa Mji Mafinga. Idadi ya wagonjwa

wahaohudumiwa kwa mwaka ni 78,520. Changamoto hii inapelekea Halmashauri ya

Mji kuelemewa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa katika Hospitali.

2

_ Kiwango kikubwa cha maambukizi ya UKIMWI na Virusi vya UKIMWI.

_ Uhaba wa watumishi kwani mpaka sasa Halmashauri ina watumishi wa Afya 185

wakati mahitaji ni watumishi 304 hivyo tuna upungufu wa watumishi 119

_ Uhaba wa dawa na vifaa tiba

2.5: Utatuzi wa Changamoto

_ Ili kupunguza msongamano katika Hospitali ya Mafinga Halmashauri inajenga

Zahanati 4 za Kisada, Ulole, Kitelewasi na Saohill pamoja na kupanua kituo cha Afya

cha Ihongole.

_ Kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya kubadii tabia, kupima kila mara na kuanza

matumizi ya dawa ARV, kwa wale wote watakaogundulika kuwa na VVU.

_ Kutenga nafasi za ajira kwenye bajeti

_ Kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na CHF/TIKA na kuongeza ukusanyaji

wa mapato ili kuweza kununua dawa na vifaa tiba.

2.0: TAARIFA YA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA IHONGOLE

Mheshimiwa Makamu wa Rais;

Kituo cha Afya Ihongole kilianza kutoa huduma mwaka 2008 ambapo kilikuwa kinahudumia

wastani wa watu 5,000 kwa mwaka. Kwa sasa kinahudumia wastani wa watu 26,032 kwa

mwaka ikiwa ni ongezeko la wastani wa watu 21,032 kutoka katika kata ya Boma na kata

jirani za Kinyanambo, Changarawe na Isalavanu. Mradi wa upanuzi wa Kituo ulianza mwezi

Novemba 2017.

Mradi huu ni juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa Malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya

Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusogeza huduma za Afya kwa wananchi yanafikiwa.

2.1: Lengo la Mradi

Mheshimiwa Makamu wa Rais;

Lengo la mradi huu ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kuimarisha Miundombinu

katika kituo ili kiweze kutoa huduma za upasuaji wa dharura na huduma ya kuongeza damu.

Ili kufanikisha hilo, mradi umelenga kuongeza majengo ya Upasuaji, Maabara, wodi ya

Wazazi, nyumba ya Mtumishi na kuhifadhia Maiti pamoja na kufanya ukarabati wa majengo

ya zamani.

2.2: Gharama za mradi:

Mheshimiwa Makamu wa Rais;

Upanuzi na ukarabati wa kituo umepangwa kutumia kiasi cha Tsh 720,000,000/=, kati ya

fedha hizo Tsh 500,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu na Th

220,000,000 ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba. Fedha hizi zimetolewa na Serikali kuu.

Mpaka sasa mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh 237,000,000 ambapo ujenzi na ukarabati

umefikia asilimia 80 kwa kutumia “Force Account”

Aidha katika utekelezaji wa mradi huu, wananchi wameshirikishwa katika hatua zote za

utekelezaji kupitia kamati mbalimbali zilizoundwa kusimamia mradi. Kamati hizo ni Kamati za

Ujenzi, Manunuzi na Ukaguzi.

Mheshimiwa Makamu wa Rais;

Hali ya utoaji huduma katika kituo cha afya ni nzuri na imeendelea kuimarika, hususani baada

ya kuongezeka kwa fedha zinazoitumika kununua dawa. Kituo kinatoa huduma za Matibabu

ya wagonjwa wa nje (OPD), wagonjwa wa kulazwa (IPD), huduma za mama na mtoto,

3

huduma za maabara na huduma endelevu kwa wagonjwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

na UKIMWI.

Baada ya kukamilika kwa mradi huduma za upasuaji mkubwa zitafanyika, huduma za

maabara zitaboreka, huduma ya kuhifadhi maiti itakuwepo na huduma ya Mama na Mtoto

zitaboreka.

2.3: Ajira zilizopatikana wakati wa utekelezaji wa Mradi

Mheshimiwa Makamu wa Rais;

Utekelezaji wa mradi huu umekuwa na manufaa kwa wakazi wa Mji wa Mafinga hasa waishio

Ihongole kwani umekuwa ni chanzo cha ajira. Mfumo uliotumika katika utekelezaji wa mradi

huu ni wa “force account” ambapo tunatumia mafundi wa kawaida (Local Fundi’s) badala ya

kuingia mikataba na wakandarasi wakubwa. Mfumo huu umeweza kusaidia upatikanaji wa

ajira kwa vijana na wananchi wa mji wa Mafinga. Jumla ya watu 138 kati yao wanawake 33

na wanaume 105 wamepata ajira na kujiongezea kipato chao kutokana na mradi huu.

3.0: Hitimisho

Mhehimiwa Makamu wa Rais;

Wananchi wa kata ya Boma na Mji wa Mafinga kwa ujumla tunapenda kutoa shukrani zetu za

dhati kwa Serikali ya Awamu ya tano kwa kuwezesha utekelezaji wa Mradi huu.

Tunayofuraha kubwa kukupokea wewe pamoja na msafara ulioongozana nao kuja kujionea

maendeleo ya kituo chetu cha Afya. Baada ya taarifa hii fupi tunakuomba uweke jiwe la msingi

katika majengo haya. Tunaamini ujio wako utakuwa ni chachu ya kuleta maendeleo katika

kuboreha utoaji wa huduma za Afya kwa Wananchi. Karibu sana na tuko tayari kupokea

maelekezo yako

Mhehimiwa Makamu wa Rais

Naomba kuwasilisha

Saada S. Mwaruka

MKURUGENZI WA MJI

HALMASHAURI YA MJI MAFINGA


Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amesema Serikali inajitahidi kujenga na kutanua vituo vya Afya ikiwa na lengo la kupunguza msongamano kwenye hospitali za Wilaya.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa kuweka jiwe la msingi  la upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole kilichopo mjini Mafinga.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Iringa ambapo leo alitembele wilaya ya Mufindi na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya kisasa na madarasa na kidato cha tano na cha sita katika Sekondari ya Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.

Akiwahutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi  la Upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole , Makamu wa Rais alisema katika kila kituo cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa Serikali imezingatia  huduma za mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, kuborsha huduma za upasuaji .

Serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na kutumia mafundi wa kawaida kujenga ilikuweza kusaidia kutoa ajira kwa vijana zaidi wa eneo husika.

Makamu wa Rais amezitaka halmashauri zisimamie utoaji na matumizi ya fedha wanazotoa kwa Vijana asilimia 5 na Wanawake asilimia 5 ili kuleta tija kwenye shughuli za maendeleo.

Makamu wa Rais alisema  “tunapozungumzia uchumi wa viwanda lazima tuwaandae Vijana tangia wadogo, tuhakikishe wanafundishwa  yale yanayohitajika”.

Makamu wa Rais aliwaambia wakazi wa Mafinga, watakapokuja tena kwenye kampeni watawataka wananchi waseme Serikali yao imewafanyia nini.

Mapema leo Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa  ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Mgololo, ujenzi ambao utagharimu  shilingi milioni  450 za kitanzania chini ya ufadhili wa kiwanda cha Mufindi Paper Mills.
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE