February 12, 2018

MKUCHIKA AKEMEA RUSHWA KWENYE IDARA YA MAADILI NCHINI

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika akiongozwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu, Mhe. Harold Reginald Nsekela wakati alipowasili katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es salaam ili kuzungumza na wafanyakazi leo.
2
Baadhi ya maofisa wa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu, Mhe. Harold Reginald Nsekela wakielekea eneo la mkutano kati yao na Waziri George Mkuchika.
3
Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu, Mhe. Harold Reginald Nsekela akisoma hotuba yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika wakati alipozungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo leo.
4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza na wafanyakazi.
5 6
Katibu Viongozi wa Siasa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Yahaya Kipacha akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika wakati waziri huyo alipozungumza na wafanyakazi katika taasisi hiyo.
7
Mmoja wa wafanyakiazi akizungumza katika mkutano huo.
8
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Filoteus Manula akizungumza jambo mbele ya waziri George Mkuchika wakati wa kikao hicho.
9
Maofiza mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza
11
Wafanyakazi mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika wakati alipokuwa akizungumza nao.
…………………………………………………………………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika amewaasa wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma kuwa waadilifu na kutojihusisha na masuala ya kupokea rushwa wakati wanapotimiza majukumu yao.
Amesema idara hiyo ni nyeti kwa kulinda maadili ya viongozi wa Umma na ni matarajio ya watanzania kuona watumishi wa taasisi hiyo hawajihusishi na vitendo vitakavyoipaka matope taasisi hiyo  na serikali kwa ujumla.
Waziri Mkuchika ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kuzungumza na wafanyakazi ambapo alisisitiza utendaji kazi wenye tija na wenye maadili wakati wowote  wanapokuwa katika majukumu yao ya kiutendaji.
Amesema “Nyinyi ndiyo mnaosimamia maadili ya viongozi na wanasiasa Mkishawishiwa kwa vyovyote vile na kujihusisha na rushwa wakati mnapokuwa katika majukumu ya kuwakagua hawa viongozi mtakuwa mmeipaka matope taasisi na wizara kwa ujumla wake.
“Sitarajii kusikia mfanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili  ya Viongozi wa Umma akipandishwa mahakamani kwa kujihusisha na masuala ya rushwa atakuwa amevunja sheria na atachukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria kama mhalifu mwingine, Lakini kikubwa zaidi ni jambo  baya kwenu lakini pia ni jambo baya kwa taasisi  kwa ujumla wake” .
“Muendelee kufanya kazi kwa uadilifu ili kujenga taasisi imara na yenye kuaminika na watanzania, maana wananchi watakaposikia mmoja wa watumishi amepandishwa mahakamani kwa kujihusisha na rushwa mtakuwa mmeitia aibu taasisi na haitaamiminika tena” amesema Mkuchika.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE