February 17, 2018

MGOMBEA WA CHADEMA KINONDONI SALUM MWALIM ALETA VITUKO AJIPELEKA POLISI ILI AKAMATWE .....

SeeBait      
Kamanda wa Polisi wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro amesema mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu hakukamatwa na Polisi, bali alijipeleka mwenyewe ili akamatwe wakati si mtuhumiwa.

Kamanda Muliro amesema mgombea huyo alijipeleka mwenyewe kwenye gari la polisi wakati si mtuhumiwa, akiamini kuwa kitendo hicho kitawafanya waandishi wa habari kumpiga picha ili ionekane kuwa amekamatwa.

“Hizi ni hadithi za abunuwasi. Hayo mambo ya kufikirika hayatakiwi kabisa. Yeye ameshapiga kura akae asubiri matokeo,” amesema Murilo.

“Amelazimisha kuchukuliwa na kuingia kwenye gari wakati si mtuhumiwa.”

Timu ya waandishi wa habari ilishuhudia leo saa 6 mchana, Mwalimu akiondoka na Polisi katika defender na kupelekwa katika kituo cha Magomeni ambapo alikaa kwa takribani robo saa na kuachiwa.

Mwalimu alifika katika kituo hicho baada ya kusikia taarifa za baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakidai kuwa kuna mtu ametoroka na sanduku lenye kura, baadaye kukamatwa na polisi akiwa na sanduku hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka polisi,  “Nilipata taarifa za kuibwa kwa sanduku hilo na nilifika eneo la tukio na kuzungumza na wakala wa Chadema, msimamizi wa uchaguzi na polisi ambao wote walikiri kuwepo kwa tukio hilo.”

“Waliniambia nijaze fomu namba 16 na kisha niondoke kwa maelezo kuwa polisi wamemkamata mtu huyo. Nikasema hilo suala haliwezekani kabisa. Wakati naendelea kuzungumza nao polisi walinichukua.”

Amesema alipofika kituo cha Magomeni alikaa kwa muda mfupi na kuachiwa huku akibainisha kuwa uchaguzi huo umekuwa na kasoro nyingi.

“Kile kituo cha Idrisa nimekikataa, yaani sikifahamu kabisa maana ushahidi upo wazi wote wamekiri sanduku kuibwa, nikitoka hapa naelekea tena huko,” amesema Mwalimu.
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE