February 20, 2018

MBUNGE WA KILOLO VENANCE MWAMOTO AULA.......

Balozi wa  wasioona  ndani ya  nchi na  nje Venance Mwamoto  akiwa katika  picha ya pamoja  na viongozi wa chama  cha  wasioona
Balozi wa  wasioona  Tanzania na nje ya Tanzania  mbunge  wa  Kilolo  Venance Mwamoto wa nne kutoka  kushoto  waliokaa akiwa na  wanachama  wa  chama  cha  wasioona Tanzania baada ya  kuteuliwa kwake  jana 
Mbunge wa  Kilolo Venance Mwamoto  kushoto  akiwa na kiongozi wa  chama  cha  wasioona baada ya  kupewa nafasi ya ubalozi  wa  chama  hicho ndani ya nchi na  nje  ya  nchi 


Mwamoto  akitoa nje ya  ukumbi 
MBUNGE wa  jimbo la  Kilolo  Venance  Mwamoto amewapongeza  chama  cha  wasooona  Tanzania  kwa  kumpa  heshima  kubwa ya  kuwa  balozi  wao  ndani na nje ya nchi .

Akizungumza  baada ya  kutunukiwa  heshima   hiyo  kubwa Mwamoto  alisema  kuwa ameipokea nafasio hiyo  kwa  mikono  miwili  kwani  siku  zote  amekuwa mtetezi wa  watu wenye  ulemavu wa ngozi (albino) na  sasa amepewa heshima ya kuwawakilisha  watu hao wasioona kama  balozi .

"  Heshima   hii  si  yangu  ni  heshima kwa  wapiga  kura  wangu wa Kilolo  kuona  hawakukosea  kunichagua  kuwa  mbunge  wao  kwani  toka  nimechaguliwa    nimekuwa   nikipewa  heshima  kubwa nje ya  jimbo la  Kilolo na ndani ya   jimbo langu "

Mwamoto  alisema  mbali ya  nafasi hiyo ya  ubunge  aliyechaguliwa na  wana  Kilolo  sasa  yeye  ni  katibu  wa  wabunge  wa CCM bungeni  Dodoma  ,pia ni  mwalimu  wa timu ya  bunge na sasa  ni balozi wa watu wasioona  Tanzania na  nje ya nchi .

Hata  hivyo  alisema  kuwa heshima   hiyo  ambayo  amepewa na   chama  cha  watu  wasiooona  Tanzania  ataitumia  vema  na  kuona  anakuwa  kiunganishi  kati yao  na jamii na  kuona  watu  wote  wasioona  wanaungana  na kuwa na sauti  moja.

Pia  aliitaka  jamii  kuendelea  kuwa  msaada  kwa  walemavu hasa  albino na  wasioona kwa  kutoa  msaada  pale  wanapohitaji  kusaidiwa kwani  alisema  baadhi ya  watu  wamekuwa  wakiwaacha  watu hao  wasioona  bila  kuwasaidia  hasa pindi  wanapovuka barabara  na maeneo  mengine ambayo yanahitaji  usaidizi  wa karibu .
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE