February 23, 2018

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA ZIARA YA KAMISHNA MKUU WA TRA BW.CHARLES KICHERE MJINI KAHAMA


picha 1
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akimuelimisha mfanyabiashara kuhusu umuhimu wa kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Ziara ya Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere Mjini Kahama, 23 Februari, 2018.
PICHA 2
Meneja Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bibi. Diana Masalla (kushoto) akiangalia namna mfanyabiashara anavyopewa huduma kuhusu namna ya kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Ziara ya Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere Mjini Kahama, 23 Februari, 2018.
PICHA 3.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) pamoja na viongozi wengine wa TRA Makao Makuu na wa mjini Kahama wakisikiliza taarifa ya mapato toka kwa Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Kituo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Isaka, Bw. Martin Kawonga (aliyesimama), 23 Februari, 2018.
PICHA 1
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (wa pili kulia) akiangalia na kutoa maagizo ya kuhifadhi eneo la ofisi ya TRA Isaka Wilayani Kahama mara alipotembelea katika ofisi hiyo kujionea shughuli za ukusanyaji mapato ya Serikali, 23 Februari, 2018
PICHA 3
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyeshika simu) akiangalia moja ya gari linalodaiwa ushuru wakati alipotembelea katika ofisi ya TRA iliyopo Isaka Wilayani Kahama kwa ajili ya kujionea shughuli za ukusanyaji mapato ya Serikali, 23 Februari, 2018.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE