February 1, 2018

MANISPAA YA IRINGA MATATANI KWA KUPUUZA AGIZO LA RAIS JUU YA MACHINGA ,UWT MKOA WATOA TAMKO

Muunguzi mfawidhi wa Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa Victoria Ntara kushoto  akishukuru kwa  msaada  wa UWT mkoa wa Iringa 
Machinga   wakiokoa mkokoteni  wao ambao mali zimechukuliwa  wakienda  kuuhifadhi  jengo la  CCM mkoa wa Iringa 
Wananchi  wakitazama  kibanda  cha  kutengeneza  simu na  kuaza  vifaa vya simu eneo la M.R ambacho kilivunjwa na  vitu  vyote  vilivyokuwemo ndani kama kompyuta ,simu  na vingine pamoja na  mita ya umeme  kubebwa 
Mwenyekiti  wa UWT mkoa wa Iringa Nicolina  Lulandara katikati  akikabidhi  vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa leo 
wauguzi  Hospitali ya  Rufaa mkoa wa  Iringa wakionyesha  vifaa  hivyo 
Mwenyekiti  wa  UWT  mkoa  akionyesha moja kati ya  vifaa  hivyo 
Baadhi ya  vifaa vilivyotolewa 
Mashine  iliyokabidhiwa 
Mwenyekiti  UWT mkoa  wa Iringa akikabidhi  moja kati ya mashine 
Misaada  mawodini kwa  wagonjwa  ikipelekwa 
Kada  Seck Kasuga  akiongozana na wanawake  wenzake kwenda  kuwafariji  wagonjwa leo 
Machinga  wakilalamika  kuvunjiwa vibanda  vyao na  kuchukuliwa mali  zao 

UMOJA  wa  wanawake  Tanzania (UWT)  mkoa  wa  Iringa umelaani  maamuzi ya Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa ya  kuharibu mali  na  kuvunja vidanda  vya biashara  vya wafanyabiashara  wadogo wadogo  maarufu  kama machinga  katika eneo la Stendi kuu ya mkoa wa Iringa .

Akitoa tamko  hilo  leo baada ya  kukabidhi msaada  wa  vifaa  tiba vyenye  thamani ya  shilingi  milioni 8.6 katika  Hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa  mwenyekiti wa UWT  mkoa Nicolina  Lulandara ,alisema   kuwa  uamuzi  uliofanywa na Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa ni  uamuzi  wa  kuwarudisha  nyuma  kimaendeleo Machinga  hao .
Mwenyekiti   huyo  alisema  kuwa UWT imesikitishwa na maamuzi hayo  mazito yaliyofanywa na  Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa kupitia mgambo wake  kwa kuvunja na  kuchukua mali  za machinga hao majira ya saa nane  usiku  wakati  wahusika wakiwa majumbani kwao .

“ Jambo  hili  tumelipokea kwa masikitiko makubwa  sana kuana machinga hao na  mamalishe ambao  walikuwa  wanajishughulisha  kupata  kipato  kuvunjiwa vibanda  vyao na  mali  zao  kuchukuliwa na Manispaa  huku  wakiwataka  kulipa faini  ya  shilingi 400,000 ndipo  warejeshewe mali  zao  “

Alisema  Pamoja na  kuwa  chama mkoa  kitatoa tamko ila kilichofanyika  wao kama wanawake  mkoa  wa Iringa  wamelaani vikali  na  kuwa  kilichofanywa ni kinyume na maagizo ya  Rais Dkt  John Magufuli  ambae aliagiza Halmashauri  nchini  kutowanyanyasa  machinga  kama  hawajawatengea  maeneo ya  kufanyia  shughuli  zao.

Wakizungumzia   tukio  hilo  kwa niaba ya  wenzao  wafanyabiashara  hao  Sila Mlimakifu  na  Anjera  Lumato  ambae ni mlemavu  wa viungo    walisema  kuwa  wao  wa  chama  chao  cha Machinga na  walikwisha  jiorodhesha na  kupewa  vitambulisho  na Manispaa ya  Iringa  inakitambua  chama  hicho  ila wameshangazwa  kuamka asubuhi  kuona vibanda  vyao  vimevunjwa na mali  zilizokuwepo  zimechukuliwa  zote .

Mstahiki   meya  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Alex  Kimbe alisema kuwa  taarifa  za  kutakiwa  kuondoka  maeneo yasiyo rasmi kama  kwenye  vichochoro na stendi ilitolewa na hakuna  mfanyabiashara  aliyeweza  kutekeleza  agizo hilo .

Hivyo  alisema  wamelazimika  kuvunja  usiku  wa manane  kutokana  na usalama  wa  mgambo  ambao  walikuwa  wakiifanya  shughuli   hiyo kwani  wangefanya  mchana  wangeweza kushambuliwa  na  machinga hao .

Kimbe  alisema  eneo  kwa  ajili ya machinga  na  wafanyabiashara  ndogo ndogo  limetengwa magari mabovu  na maeneo ya  ngome Pamoja  na Kitwiru  ila   machinga hao  hawataki kwenda .

Katika  hatua  nyingine UWT  mkoa  wa  Iringa imekabidhi vifaa tiba  mbali mbali zikiwemo  Suction mashine ,Nabulaiza , Injection Ambliciline  pia  nmafuta  ya kupaka  kwa  wagonjwa ,sabuni na vitu ningine  vyote  vikiwa na thamani ya  shilingi  milioni 8,637,000.

Katibu  wa  UWT  mkoa  wa Iringa Chiku Masanja  alisema msaada  huo  umetolewa  na  UWT  kupitia  wadau  wake mbali mbali lengo  likiwa ni  kutatua  changamoto ya  vifaa  tiba katika Hospitali  hiyo ya  Rufaa mkoa  wa Iringa hasa kunusuru  maisha ya mama na mtoto .

TAZAMA  VIDEO  ZA MATUKIO YA MACHINGA KUVUNJIWA NA TAMKO LA  UWT MKOA 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE