February 19, 2018

MAKAMU WA RAIS AWASILI MWANZA KWA ZIARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Mwanza jana jioni na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kesho mkoani Simiyu.
Katika ziara hiyo itakayoanza kesho tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018, Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi  wa maji Kiloleli na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na wanachi Lamadi .
Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa  katika eneo la Nyaumata.
Miradi mingine ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za Mjini.
Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya (Meatu)
Tarehe 21, Makamu wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda Tanzania kasha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na kusalimia wananchi, kufungua jingo la upasuaji  la Samia Suluhu  Hassan katika Hospitali ya Wilaya  ya Maswa na kuzungumza na wananchi katika viwanja vya nguzo nane.
Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali  ya 34 ya Chuo Kikuu Huria .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE