February 11, 2018

MAKAMU WA RAIS APONGEZA UFADHILI WA MAKAMPUNI YA MPM KWA UJENZI WA MAABARA YA KISASA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi      Mgololo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Maabara ya shule ya  Sekondari Mgololo, wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
MAKAMU wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amezindua ujenzi wa jengo la maabara linalojengwa na kiwanda cha karatasi Mufindi (MPM ) kwa kiasi cha shilingi milioni 450.


Akiwatubia wananchi wa Mgololo wilayani Mufindi mkoani Iringa Leo,makamu wa Rais mbali ya kupongeza jitihada za Kiwanda cha MPM kwa kusaidia ujenzi huo na kuhidi kusaidia sekta ya afya na elimu.

Alisema serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na wawekezaji ikiwemo kampuni hiyo ya MPM katika kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo na kutaka wananchi kuishi vema na wawekezaji hao.

Kwani alisema miradi ambayo MPM imejitolea kusaidia ni miradi mikubwa na italeta chachu kubwa ya ukuzaji wa uchumi wa wilaya ya Mufindi huku akiwataka wananchi kuitunza miradi hiyo baada ya kukabidhiwa jukumu la kuifanyia matengenezo na kuitunza  si jukumu la mwekezaji tena.

Makamu wa Rais alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kutekeleza ujenzi wa barabara ya lami toka Mafinga kuelekea kiwanda cha MPM na barabara nyingine zote ambazo zipo kwenye ilani ya uchaguzi .

Kwani alisema kwa sasa barabara za Mufindi ambazo alizipo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM zimekwisha fanyiwa upembuzi yakinifu.

Awali wabunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamudu Mgimwa na Mbunge wa Mufindi kusini Mendard Kigola walimuomba makamu huyo wa Rais kufikisha kilio cha wananchi wa Mufindi juu ya ubovu wa miundo mbinu.

Akitoa akisoma taarifa ya mradi wa jengo la maabara ya shule ya sekondari ya Mgololo ,mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mufindi Prof Riziki Shemdoe 

Alisema kwa ujenzi huo unatarajiwa kuwa na miundo mbinu kama maabara tatu za sayansi ,chumba kimoja cha kompyuta ,vyumba vitano vya maabara kwa ajili ya mikondo ya kidato cha tano na sita.

Kuwa mradi huo ulinza January mwaka 2016 utakamilika mwezi Aprili 2018 utagharimu kiasi cha milioni 325 kwa awamu ya kwanza na kuwa awamu zote mbili ya kwanza na ya pili mradi huo umefadhiliwa na MPM .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE