February 9, 2018

MAKAMU WA RAIS APONGEZA JITIHADA ZA ASAS GROUP IRINGA

Mkamu  wa  Rais  Samia  Suluhu  Hassan  akimkabidhi  hati ya  pongezi  Feisal  Asas  baada ya  kufungua zahanati  iliyojengwa  kijiji  cha  Kising;a  kwa  ufadhili  wa  kampuni  ya Asas  Group  kwa  kiasi cha  shilingi  milioni 125  leo 
Mjumbe  wa  NEC Taifa  Salim  Abri  Asas  akitoa  neno  mbele ya makamu  wa Rais  
Mbunge  wa  Kalenga  Godfrey  Mgimwa  akimsikiliza  kwa makini  waziri  wa Ardhi  ,nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam  Lukuvi  (kulia)
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  kushoto  akiwa na  viongozi  mbali mbali  wa  mkoa  wa Iringa  wakijiandaa  kumpokea makamu  wa  Rais leo 
Makamu  wa  Rais  Samia  Suluhu  Hassan  akisalimiana na mjumbe wa  NEC  Salim  Abri  Asas  leo 
Waziri  wa  Ardhi  Nyumba na maendeleo ya makazi  Wiliam Lukuvi  akisalimiana na  makamu  wa  Rais 
Mbunge  wa  Kalenga  Godfrey  Mgimwa  akisalimiana na makamu  wa  Rais 
Feisal  Asas  akisalimiana  na makamu  wa  Rais 

Na  matukiodaimaBlog 

MAKAMU  wa  Rais  wa  jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  Samia  Suluhu  Hassan  amepongeza  jitihada   kubwa  zilizofanywa na kampuni ya  Asas Group  ya  mkoani  Iringa kwa  kuwajengea  wananchi  wa  Kising’a  wilaya ya  Iringa   vijijini   Zahanati .

Akitoa pongezi   hiyo  leo  wakati  wakati  wa  ufunguzi  wa  Zahanati   hiyo  mamamu  wa   Rais amesema  kuwa   jitihada  zilizofanywa na kamapuni ya  Asas Group   ni  jitihada  kubwa   zenye  malengo ya  kusaidia kuokoa  uhai  wa  wananchi wa  kata ya  Kising’a .

“  Kilichofanywa na  kampuni ya  Asas Group  ni  utekelezaji  wa ilani ya  CCM kwa  vitendo  pia kujengwa  kwa  Zanahanati  hiyo  iwe  ni  safari ya  kuelekea  ujenzi  wa  kituo  cha  afya   hivyo   wilaya  na  wadau  pamoja na  wananchi  wanayokila sababu  ya  kujipanga  ili  kuona safari  hiyo  inatimia  “

 Alisema  kuwa  vijiji vitatu  vinavyotumia  zahanati   hiyo   kuna  haja  ya  kuendelea   kuungana  pamoja na  mdau  ili  kuona  ujenzi  wa  kituo   cha  afya  unaendelezwa  na kuifanya  za hanati  hiyo  kuwa  kituo  cha  afya .

“  Jitihada   kubwa  imefanyika  katika    zahanati hii  ila  bado  kuna  haja ya  kuhakikisha  upanuzi   unafanyika  zaidi  ili  kuifanya  kuwe  na  chomba  cha  upasuaji  na  wodi  zaidi  kwani  nimeonyeshwa  sehemu ya  kujifungulia  wanawake  ila  lazima  kuhakikisha   ujenzi  wa  wodi  zima la  akina mama  kwa  ajili ya  kujifungulia  linaanzishwa “

Aidha  alisema  kuwa  iwapo  wananchi  watajitoa kwa  nguvu  kujenga   kituo  cha afya  serikali itauna  mkono  jitihada   hizo  pamoja na  kuendelea  kupiga magoti  kwa  Asas Group   ili  kuona  anaendelea  kusaidia  zaidi .

Pia  makamu  wa  Rais  amewataka  wananchi  kujiunga na bima ya  afya  ili  kuweza  kutibiwa  wakati  wote ambao  watakuwa na matatizo .

Wakati  huo  huo  makamu  wa  Rais  ameahidi  kusaidia kupambana    kutatua  kero ya maji  katika    tarafa ya  ismani  ikiwa  ni  pamoja   na kutafuta   wahisani  wa  kusaidia  mradi  wa  visima   wakati  serikali  inaendelea  na ufumbuzi  wa  kudumu  wa  kutafuta  pesa  kwa  ajili ya  kujenga mradi mkubwa wa maji  kutoka  mji Iringa hadi  Ismani  ama  kutafuta  vyhanzo  vya  uhakika  kutoka tarafa ya  Ismani .

Kwa  upande  wake  mbunge  wa  jimbo la  Ismani  Wiliam  Lukuvi  ambae  ni  waziri  wa  ardhi  ,nyumba na maendeleo ya makazi alisema  kuwa  jitihada  kubwa  imeendelea  kufanywa na  serikali ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais  Dkt  John Magufuli   imekuwa  mbele  kutekeleza  miradi  mbali mbali ya  kimaendeleo  na  kuwa ni amani  kubwa  suala la  kero ya  maji litatafutiwa  ufumbuzi  wa  kudumu .

“ serikali  hii  ya awamu ya  tano   imejitiahidi  kwa  kupeleka  umeme  katika  vijiji  vyote  vya  jimbo la  Ismani  na  kuwa na  tayari  wataalum   wa  kusambaza  umeme  wamekwisha  anza  kazi katika  vijiji  vyote  vilivyopo  jimboni  kwake .

 Mjumbe wa  Halmashauri  kuu ya  CCM  Taifa  Salim  Abri  Asas  anayewakilisha mkoa  wa  Iringa alisema  kuwa  kazi  kubwa  kubwa kwake  ni  kuendelea  kuipigania  CCM  na  kuona  utekelezaji wa  ilani ya  CCM unafanyika  na  kuwa  kamwe  mkoa  wa  Iringa  kisiasa  hautateteleka.
“  Tupo  hapa  kuitetea  serikali  yetu  na  mtu  yeyote  atakaye ikwamisha  serikali  tupo  tayari  kuona  tunashughulika nae  .
Akitoa  taarifa  ya  ujenzi  wa  Zanahati   hiyo  mkurugenzi  mtendaji  wa Halmashauri ya  Iringa Robert Masunya  alisema  kuwa   kampuni ya Asas   Group  imechangia  kiasi  cha  shilingi  milioni 125 .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE