February 19, 2018

NAIBU WAZIRI APIGA MARUFUKU KAMPUNI ISIYO NA LESENI KUFANYA UCHANJUAJI MGODI WA NYAKAVANGALA ,AAAGIZA MGODI KUFUNGULIWA ....


WIZARA  ya  madini   imetoa   muda  wa  wiki  mbili kwa  wachimbaji  wadogo  wa mgodi  wa madini ya  dhahabu   wa Nyakavangala  wilaya  ya  Iringa mkoani  Iringa kufanya  marekebisho  ya  kiusalama katika machimbo  hayo ili  ufunguliwe  iwapo  hakutakuwepo  usalama  serikali haitaufungua  mgodi huo .

Huku   akipiga  marufuku  kampuni  yoyote  isiruhusiwe  kufanya  kazi ya  kuchinjua makinikia  ya madini  eneo  hilo  bila  kuwa na  leseni na  kama  wapo wanaofanya   hivyo kusimamishwa  mara  moja  kuanzia  sasa .

"Uchenjuaji  una  athari  kubwa  kwa mazingira    hivyo lazima  kampuni inayotaka  kufanya uchenjuaji  kukaguliwa na  kuwa na leseni halali  ya  kufanya kazi  hiyo "

  Agizo hilo limetolewa   leo  na  naibu  waziri wa Madini Dotto  Biteko   wakati akiwahutubia  wachimbaji  hao   mara  baada ya  kutembelea na  kukagua  maeneo  yote  yanayochimbwa madini  katika  eneo hilo la Nyakavangala .

Naibu  waziri   huyo  alisema  kuwa serikali ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais  Dkt  John Magufuli ni  serikali ya  wanyonge  na  hivyo  isingependa  kuona   wachimbaji hao  wanaendelea  kushinda  bila  kufanya kazi kutokana na  kufungwa kwa muda kwa  mgodi   huo  kwa  ajili ya  kiusalama .

"  Serikali  ipo  kwa  ajili ya  kuwasaidia  kuona  mnatoka katika uchimbaji mdogo  na  kwenda kuwa  wachimbaji  wa kati  ama  wakubwa     japo  serikali  haitakubali  kuona  hata  mtu  mmoja  anapoteza maisha   kutokana na sababu  za  kiusalama  mgodini  hivyo  hatupo  tayari  kuona mtu hata  mmoja anapoteza maisha  kwa  kufukiwa  na  kifusi  ndani ya mgodi  wekeni  usalama  mzuri wa  mashimo yenu  mtu  akipoteza maisha  mgodi  utafungwa "

Alisema  kuwa lazima  zoezi  la  kuboresha  mambo ya  kiusalama  migodini  lifanyike  ndani ya muda  mfupi  ili  ikifika  wiki  mbili  kuanzia  leo basi  mgodi  huo  ufunguliwe na  kuanza  kufanya  kazi kama  awali .

Hata   hivyo  alitaka   kamati ya  usimamizi  wa  mgodi   huo  kusiomamia   taratibu  za  uchimbaji  wa madini na  kuwa  mchimbaji  yeyote ambaye  atakiuka  taratibu  za uchimbaji  madini  atafutiwa  leseni  yake na  wale  .

Aidha  alisema kutokana na wataalamu  wa  madini  kudai  kuwa  tayari  taratibu  hizo  zimekamilika  ofisi  yake  itatuma   mtaalamu  wa  usalama  mgodini  ambae  atakagua   shimo  moja  baada  ya  jingine kabla ya  kufunguliwa  kwa  mgodi  huo .

Kuwa     wizara  yake  inakamilisha  zoezi la  kuanza  kutoa  leseni kwa  wachimbaji   wadogo  wakiwemo  wachimbaji wa  mgodi huo  wa  Nyakavangala  ambao  wapo  mbioni  kupewa  leseni  zao  wakati  wowote .

" Rais   wetu  Dkt  Magufuli  ametoagiza  kuwa  simamia  wachimbaji  wadogo  ili  wakue  na  sisi    wasaidizi  wake  tunawasaidia  kuona  mnafanya kazi bila  kunyanyasika  ila  tunataka  usalama  wenu  kwanza "

Katika  hatua  nyingine  naibu  waziri   huyo  ameagiza  uchunguzi  kufanyika  ili  kujulikana  milioni zaidi ya 56  ambazo  zinadaiwa  zimeliwa  na  mmoja kati ya wakurugenzi wa mgodi  kwa  kuuza mawe  kinyemela  na  kuwa  wahusika  wote  tabanwe na  kurudisha  pesa  hizo .

Aidha  Biteko alisema  kwa  wasimamizi  wa mgodi  huo  wa Nyakavangala  pamoja na  kupewa  leseni  watatakiwa  kulipa  gharama  zote  za mrahaba ambazo  walikuwa  hawalipi  serikalini .

Kwa  upande  wake  mkuu wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza alisema  kuwa  suala la unyanyasaji  wa wanawake  katika  mgodi  huo  limeendelea  kujitokeza kwa baadhi ya  watu  kuwavua nguo  wanawake na  kuwalaza  katika  mashimo  yao  kwa  imani  za kupata  madini  mengi  zaidi .


Pia  alisema  hatakubali  kuona  wachimbaji hao  hawalipi kodi kwani  kodi ndio  inayowezesha  serikali  kuwaboreshea  huduma  mbali mbali  ikiwemo  miundo mbinu ya  kuelekea katika mgodi  wao na huduma  nyingine za afya 

Akitoa  taarifa  ya  mgodi  huo  wa Nyakavangala  kwa naibu  waziri  mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya  Iringa Robert Masunya  alisema  kuwa  machimbo  hayo  usimamizi na uendeshaji  ulianza  tarehe 23  /5/2017 kwa watu  waliokuwa wameomba  leseni  ya uchimbaji katika  kijiji cha  Nyakavangala  ambao ni Thomas Masuka  na  wenzake  Hilary Malima   na  Elias Lupituka  ili  kuondokana na uchimbaji Holela uliokuwa  unahatarisha   usalama  katika  machimbo hayo  na  kwa  sasa  kuna  wachimbaji  wawili wenye  leseni ambao  wanaendelea na  uchimbaji .

Alisema kupitia  sheria  ndogo  za  halmashauri  imekusanya jumla ya  shilingi milioni 52,857,990 kwa kipindi  cha Juni 2017  hadi  January 2018 pia kuna michango ya  maendeleo iliyotolewa  na  msimamizi wa machimbo ya madini kwa  Halmashauri  ya  wilaya ,Kijiji cha  Nyakavangala na  ujenzi   wa  kituo  cha  Afya  Mkulula  kimejengwa  ambapo  Halmashauri  ya wilaya imechangia milioni 17,1000,000 na  kijiji  cha Nyakavangala  kimechangia milioni 36,810,000 na kituo  cha Afya Mkulula  shilingi milioni 64,929,200

Pia  alisema  mgodi  huo  umepata  ajali mara  tatu kutokana na usalama  mdogo  uliopo katika  mashimo na  kusababisha  vifo hali  iliyopelekea  mgodi  kufungwa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE