February 24, 2018

Korea Kaskazini yalaani majaribio ya makombora ya Marekani na Japan

 Korea Kaskazini yalaani majaribio ya makombora ya Marekani na Japan
Serikali ya Korea Kaskazini imetoa taarifa ya kulaani vikali majaribio ya makombora yaliyofanywa na Marekani na Japan.

Kamisheni ya amani ya Korea Kaskazini jana Ijumaa ilisema kuwa, majaribio hayo ya makombora kati ya nchi hiyo ni harakati chafu ya kichokozi na ya kupenda kujitanua ambayo inaweza kuzusha vita hatari katika eneo hilo.

Shirika la Habari la Yonhap News la Korea Kusini limetangaza kwamba, maneva hayo ya pamoja kati ya Marekani na Japan ambayo yalianza jana Ijumaa, yataendelea kwa muda wa wiki moja.
Kim Jong-Un, Kiongozi wa Korea Kaskazini
Mbali na kufanyiwa majaribio makombora, maneva hayo yatawashirikisha pia askari wa vikosi vya anga, nchi kavu na baharini.

 Awali Japan iliiomba Korea Kusini kushiriki katika maneva makubwa ya nchi tatu, yaani Marekani, Japan na Korea Kusini, hata hivyo Seoul ilikataa kwa kukhofia kuharibu uhusiano ambao umeanza kuborea kati yake na Korea Kaskazini.

Siku ya Alkhamisi Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini alinukuliwa akisema kuwa, baada ya kumalizika michuano ya ya msimu wa baridi kali inayoendelea huko Pyeongchang, Korea Kusini, Seoul itajikita katika kufanya mazungumzo zaidi na Korea Kaskazini kwa ajili ya kutatua maudhui ya silaha za nyuklia za nchi hiyo. 
Bi Kang Kyung-wha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini
Bi Kang Kyung-wha, aliongeza kwamba, Seoul itaendelea na juhudi zake hizo za kidiplomasia za kukaa meza moja na Pyongyang ili kuiepusha Rasi ya Korea na silaha za nyuklia.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE