February 24, 2018

Komandi ya kijeshi ya Imarati yashambuliwa kwa kombora la belestiki Yeme

 Komandi ya kijeshi ya Imarati yashambuliwa kwa kombora la belestiki Yemen
Jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen zimeshambulia kwa kombora la belestiki komandi wa kijeshi ya wanajeshi vamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) katika mkoa wa Ma'rib nchini Yemen.

Mwaka 2015, Saudi Arabia kwa kushirikiana na baadhi ya nchi za Kiarabu hasa Imarati na kwa baraka kamili za Marekani, Israel na baadhi ya madola ya Magharibi ilianzisha mashambulizi makubwa ya kila upande katika nchi maskini ya Yemen.

Hadi hivi sasa makumi ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo ya Waislamu wameshauawa na kujeruhiwa na mamilioni ya wengine wamekuwa wakimbizi.

Wananchi wa Yemen kupitia jeshi lao na kamati za kujitolea vya wananchi wamelazimika kujihami na kusimama kidete kupambana na wavamizi wa nchi yao, hivyo wamekuwa mara kwa mara wakijibu mashambulizi wanayofanyiwa.
Maarib
Saudia haikuwabakishia chochote wananchi wa Yemen isipokuwa magofu

Televisheni ya al Masira ya Yemen imetangaza kuwa, katika opereseheni ya jana Ijumaa, vikosi vya Yemen vilishambulia kwa kombora la balestiki komandi ya kijeshi ya wanajeshi vamizi wa Imarati katika mkoa wa Ma'rib, katikati mwa Yemen.

Vile vile jeshi la Yemen na kamati za kujitolea za wananchi zimefanikiwa kuangamiza mamluki 18 wa Saudia na kujeruhi makumi ya wengine katika eneo la al Sarwah, mkoani Ma'rib.

Itakumbukwa kuwa juhudi mbalimbali zinaendelea kwa shabaha ya kukomesha uvamizi na mashambulizi ya kikatili ya kundi vamizi la nchi zinazoongozwa Saudia huko Yemen. 

Kwa upande wake, harakati ya Answarullah ya Yemen imependekeza kuundwa kamati maalumu ya mapatano na kupewa nafasi wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua rais na wabunge kwa namna ambayo wananchi na vyama vyote vya kisiasa vya Yemen vitashiriki kwa uhuru kamili kwenye chaguzi hizo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE