February 21, 2018

KAMPUNI ZA MADINI TANZANIA ZAAMRIWA KUTUMIA BENKI ZA WAZAWA PEKEE

 Benki za kigeni zimetengwa na kanuni mpya za uwekezaji sekta ya madini
Wawekezaji katika sekta ya madini nchini Tanzania wanakabiliwa na sura mpya ya uwekezaji baada ya serikali kutunga kanuni mpya zitakazoongoza utekelezaji wa sheria mpya za madini nchini humo.

Mwaka jana, Tanzania ilipitisha sheria zilizoonekana kudhibiti vikali utendaji wa wawekezaji huku serikali ikitarajia kuvuna faida ya kutosha kutoka katika rasilimali kubwa ya madini iliyopo nchini.

Mathalani, sheria hizo zinatoa fursa kwa serikali kupitia upya mikataba yote ya madini na kutilia mkazo kwa kampuni shughuli za uchakataji madini kufanyika nchini.

Sheria hizi pia zimebainisha wazi kwamba rasilimali madini ni mali ya taifa, kinyume na ilivyokuwa hapo awali ambapo hakuna sheria iliyokuwa imeweka wazi umiliki wa madini kwa taifa.

Pamoja na mambo mengine, kanuni hizi mpya ambazo kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Madini zimeanza kufanya kazi tangu mwezi uliopita, zinatoa kipaumbele si tu kwa taasisi za fedha na huduma za kisheria za Kitanzania lakini pia ajira kwa Watanzania.

Kuhusiana na huduma za kifedha, kanuni mpya zinataka makampuni ya madini kufungua akaunti na kuweka fedha zao katika benki za wazawa.

"Benki ya wazawa ni ile inayomilikuwa na wazawa kwa asilimia 100 ama ile ambayo Watanzania wanamiliki hisa nyingi zaidi", inafafanua sehemu ya kanuni hizo

Hii inaziengua benki kadhaa za kigeni kufanya biashara katika sekta ya madini. Baadhi ya benki za kigeni zinazofanya kazi nchini ni pamoja na Stanbic, Barclays, Standard Chartered na ile ya Afrika Kusini ya First National Bank (FNB)

Kanuni zinataka pia utoaji wa leseni za uchimbaji madini utoe kipaumbele kwa kampuni za kizawa kampuni zitakazoshindwa kutekeleza kanuni hizi zitatozwa faini ya hadi dola milioni 5 za kimarekani ($5 Milioni).

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE