February 21, 2018

JAFFO ATOA NENO KWA WADAU WA ELIMU

 Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akipokea madawati 70 kutoka Mamlaka ya Udhibiti
wa Chakula na dawa(TFDA).

 Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Mvomero
Suleiman Saddiq na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk.Steven
Kebwe.

 Viongozi wakikagua madawati yaliyotolewa na Mamlaka
ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA).

Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wengine wa mkoa wa Morogoro.
 …………………………………………………….
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo amewataka wadau mbalimbali kuendelea kuunga
mkono juhudi za serikali ya kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu
bora.
Jafo ameyasema hayo
wakati akipokea msaada wa madawati 70 kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na
Dawa(TFDA) kwa ajili ya shule za Halmashauri ya wilaya ya Mvomero mkoani
Morogoro.  
Jafo amewaomba wadau
mbalimbali zikiwemo Taasisi za serikali na Taasisi binafsi kuunga mkono juhudi
za Rais Dk. John Magufuli anazozifanya katika sekta ya elimu ambapo takriban sh.
bilioni 23 hutolewa kila mwezi kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo. 
Kwa upande wake, Mbunge
wa Mvomero
Suleiman Saddiq ameiomba serikali na wadau kuendelea kuzisaidia
shule za Mvomero kwa upande wa madawati na vyumba vya madarasa.
Amesema programu ya
elimu bila malipo imesababisha wazazi wengi kuwapeleka watoto wao shuleni hivyo
kusababisha madawati na vyumba vya madarasa kuwa ni changamoto kubwa wilayani
humo.
Pia amempongeza Waziri Jafo katika jitihada zake za kuwahudumia watanzania.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE