Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imewataka waganga wakuu wa
mikoa na wilaya kuhamasisha jamii katika kuwaibua wagonjwa wa akili
kuwapeleka katika vituo vya afya ili wapatiwe matibabu kwa madai hiyo ni
bure.

Licha Ya Serikali Kueleza
Kutotambua Idadi Kamili Ya Wagonjwa Wa Akili Nchini Tanzania, Inakadiriwa Kuwa
Wagonjwa Wa Akili Ni Asilimia Moja Ya Idadi Ya Watanzania Wote Wanaokadiriwa
Kufikia Takribani Watu Milioni 50.
Kwenye Vikao Vya
Bunge Vinavyoendelea Mjini Dodoma Hii Leo, Naibu Waziri Wa Afya Nchini, Dk
Faustine Ndugulile Ametaja Takwimu Hizo, Kwamba Tanzania Itakuwa Na Wastani Wa
Watu 500,000 Ambao Ni Wagonjwa Wa Akili.
Kati Ya
Kadirio La Wagonjwa Hao Ni Asilimia 48 Tu Ndio Wanafika Kwenye Vituo Vya
Kutolea Huduma Za Afya, Asilimia 24 Wanapelekwa Kwa Waganga Wa Kienyeji Wakati
Asilimia Iliyobaki Wanapelekwa Katika Huduma Za Kiroho.
Naibu Waziri Huyo
Ametoa Kauli Hiyo Wakati Akijibu Swali La Msingi La Mbunge Wa Morogoro Kusini, Prosper
Mbena Aliyetaka Kujua Ni Kwa Nini Serikali Haina Utaratibu Wa Kuchukua Wagonjwa
Wa Akili Walioko Mitaani.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE