February 1, 2018

CHAMA CHA WAMILIKI WA MBWA TANZANIA KUZINDULIWA KESHOKUTWA


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania  Canine
Association Ltd (TCAL) Sinare Sinare, akizungumz na waandishi wa habari katika
Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jana wakati akitangaza uzinduzi rasmi wa
Chama cha Wamiliki wa Mbwa utakaofanyika katika Viwanja vya Leaders Club
Kinondoni kesho. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Inspector General wa
Polisi (IGP) Simon Siro. Kushoto kwake ni Wajumbe wa Kamati ya uzinduzi huo,
Felician Bolu na Deo Rweyunga. (kushoto) ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Mbwa
na Farasi, Dkt. Egyne Emmanuel. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Mkutano ukiendela….
Na Amina
Kasheba, Dar (DSJ)
INSIPEKTA wa
polisi (IGP) Simon Siro atanatarajia kuwa
mgeni ramsi katika uzinduzi wa chama cha mbwa kilichoundwa na Tanzani Acanine  Assoation limited (TCAL) wafuga mbwa wa Mkoa
wa Dar es salaam.
Uzinduzi huo
unatarajia kufanyika Febuari 3 mwaka huu na kushirikishwa na wasio kuwa
wanachama ili kuleta ushirikiano katika masuala ya wafugaji Tanzania.
Akizungumza
na mwandishi  wa habari katika Ukumbi wa
Idara ya Habari Maelezo Dar es salaam jana,  Mkurungenzi   wa kampuni
ya Tanzania Acanine Association Limited (TCAL) Dk. Sinare Sinare,  alisema dhumuni ya kuanzisha chama hicho ni
kuwakutanisha wadau mbalimbali na wamiliki wa mbwa Tanzania ili kujenga
ushirikiano baina ya wanachama wenyewe kwa lengo la kusimamia na kushauri
kuhusu uzalishaji mbwa bora.
Aidha
alisema wameamua kuanza kuhamasisha ufugaji bora wa mbwa ikiwa ni pamoja na
kushawishi ufugaji unaojali maslahi a faida  ya wanyama mbwa katika jamii na kutoa ushauri
wa jinsi ya kusimamia ili kupata zao bora la Mbwa.
 “Dhumuni la kuanzisha chama hicho ni
kuwakutanisha wadau na wamiliki wa mbwa Tanzania, ili waweze kuwa na sauti ya pamoja
kama wamiliki wa Mbwa Tanzania,
Aliongeza
kuwa katika uzinduzi huo hakutakuwa na kiingilio ambapo mtu yoyote anaruhusiwa
kuhudhuria na kujionea michezo mbalimbali ya Mbwa na Farasi.
Katika
kusherehesha uzinduzi huo pia kutakuwa na maonyesho mbalimbali kutoka Kikosi
cha mbwa ambao wataonyesha uwezo wa mbwa wao katika kulinda uslama wa raia na
mali zao, pamoja na michezo ya farasi.

Baada ya
uzinduzi huo itakuwa ni sehemu ya maandalizi ya maonyesho makubwa ya mbwa
yanayotarajia kufanyika Juni 6 mwaka huu
na kushirikisha washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE