February 6, 2018

CHADEMA IRINGA MJINI INAKWAMISHA WAWEKEZAJI WA VIWANDA -MICHAEL MLOWEWAKATI serikali  ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais Dkt  John  Magufuli  ikija  na mpango  mkakati wa  kuongeza  idadi ya  viwanda  vidogo  ,vya kati na  vikubwa kwa  kila mkoa  kuwa na  viwanda  100 kada  wa chama  cha mapinduzi (CCM)  Michael Mlowe aibuka na  kudai  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa iliyopo  chini ya  Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  inakwamisha wawekezaji kuwekeza viwanda .

Mlowe  mwenye  degree moja ya michezo ambae  alipata  kuwa  mmoja  kati ya makada  wa CCM waiojitokeza kuwania ubunge jimbo la  Iringa mjini katika  mchakato  wa  ndani ya  CCM mwaka 2015 anasema  kuwa inashangaza  kuona  uongozi  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  ukiwasumbua wafanyabiashara  ndogo ndogo  maarufu kama Machinga  ambao wameamua  kuwekeza  katika  shughuli za  kijasiliamali ila  wanavunjiwa vibanda  vyao  vya  biashara tena  usiku  wa manane  na  kuchukuliwa  mali  zao.katika kutekeleza azma ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda, mkoa wa Iringa umepewa mwaka mmoja kuhakikisha unaanzisha viwanda si chini 100.


“  Hayo ni malengo, lakini utekelezaji wake unategemea sana wadau wote kwa  asiwepo  mtu  wa kuweka mazingira ya  kuwatisha wawekezaji kama inavyofanya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa”

..........................ENDELEA  KUFUATILIA .............................. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE