February 2, 2018

TANZIA :KINGUNGE NGOMBALE MWIRU AFARIKI DUNIA


Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Kingunge Ngombale-Mwiru, 87, amefariki dunia, jamaa zake wameiambia
Mzee Kingunge amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mwanasiasa huyo mkongwe alilazwa hospitalini mwanzoni mwa Januari akiuguza majeraha ya kushambuliwa na kung'atwa na mbwa nyumbani kwake na akafanyiwa upasuaji.
Alikuwa mmoja wa viongozi wa muda mrefu na miongoni wa watu waliokuwa na ushawishi katika Chama cha Mapinduzi (CCM) hadi alipojiuzulu kutoka kwenye chama hicho Oktoba 2015 akilalamikia alichosema ni ukiukaji wa katiba ya chama hicho.

Kabla ya kujiuzulu, alikuwa amesema kwamba hakuwa amefurahishwa na utaratibu uliotumiwa kumteua mgombea urais wa CCM mjini Dodome Julai mwaka huo.
Hata hivyo, aliahidi kutohamia chama kingine.

Bw Kingunge alikuwa amehduumu katika CCM tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1977.
Mke wake, Peras, alifariki dunia mwezi uliopita akitibiwa pia Muhimbili baada ya kulazwa kwa miezi kadha.
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikuwa amefika katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumjulia hali Mzee Kingunge mwanzoni mwa mwezi Januari.

BWANA  AMETOA  NA BWANA  AMETWAHA JINA  LAKE  LIHIMIDIWE  DAIMA


Unaweza  kupata  matukio  mbali  mbali kila  baada ya  dakika  25  kupitia chanel yetu ya  Youtube ;Matukiodaima   tembelea  sasa  kisha bonyeza  Subscriber na alama  ya  Kengele itakayotokea hapa  utakuwa  umejiunga  nasi  ,pia  kuendelea  kupata  habari  kupitia blog hii ingia Play Store andika MatukiodaimaBlog kicha Pakua APP yetu  wengi  wanajiunga  nasi  bado  wewe kwa  mawasiliano iwapo  una habari au  tangazo piga  simu 0754026299

 Magufuli

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE