February 2, 2018

BASI LA THMEED LAUA MKOANI TANGA


_MG_9736
Basi la kampuni ya Tahmeed  limepata ajali baada ya kupinduka  eneo la  Kitumbi Kata ya Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga na taarifa za awali zinasema ajali hiyo imesababisha kifo cha mtu mmoja na  wengine  20 kujeruhiwa wakati  dereva wa basi hilo akimkwepa mwendesha pikipiki.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoani Tanga
,Kamanda Edward Bukombe amesema ni kweli ajali hiyo imetokea ikihusisha basi
la kampuni ya Tahmeed ambalo lilikuwa likitokea Mombasa kwenda Dar es
Salaam.
Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo,Kamanda Bukombe alisema kwa taarifa
za awali ni hizo hivyo wanaendelea kufuatilia na baadae atatoa
taarifa rasmi kuhusiana na ajali hiyo.
 Hii ni ajali ya pili kutokea katika kipindi cha wiki moja
index
Baadhi ya majeruhi wakiokolewa kutoka katika ajali hiyo ya basi la Tahmeed.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE