February 12, 2018

ATAKAYE KWAMISHA MRADI WA REGROW KIKIONA - MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Mzee  kaundama wakiwa na wananchi katika uzinduzi wa mradi wa Regrow

Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kulia 
Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Arif Abri akiwa katika uzinduzi wa mradi wa Regrow 

Wadau wakiwa banda la bonde la Maji Rufiji 
Wananchi wakitembelea banda la Boma 
Wadau wakiwa katika banda la Boma 
Wadau wakitembelea mabanda mradi wa Regrow 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa salamu za Mkoa Leo

Kada wa CCM Michael Mlowe na Naibu meya Dady Igogo kulia wakiwa katika uzinduzi  wa Regrow 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la  mradi wa REGROW na Mikataba ya Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa ,kushoto ni  waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Wiliam  Lukuvi na  kulia ni mwakilishi wa benki ya Dunia  Bella Bird na mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  ,mwenye shati la  kijani ni mjumbe wa NEC Taifa  Salim Abri Asas 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW.
Baadhi ya  wananchi  walioshiriki  uzinduzi wa mradi wa Regrow Iringa 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa
Na  MatukiodaimaBlog 

MAKAMU   wa  rais  wa  jamhuri ya    muungano wa  Tanzania  Samia Suluhu  Hassan  amewataka   watumishi  wa  taasisi  zote  zitakazohusika  na utekelezaji  wa mradi  wa  uimarishaji  usimamizi  wa  maliasili  na  kuendeleza  utalii kanda ya  kusini mwa Tanzania (REGROW)  kuifanya  kazi  hiyo kwa  weledi  na umakini  .

Akitoa   ahizo  hilo  jana  wakati wa  uzinduzi  wa mradi  wa  REGROW  katika  eneo la  kihesa  kilolo mjini  Iringa makamu  wa  Rais  alisema  kuwa  ni  vema  utekelezaji  wa  mradi huo  kusimamiwa kwa weledi mkubwa  ili  kufikia malengo yaliyotarajiwa na  serikali  pamoja na  wahisani  wa mradi huo .

“Nawasihi  pia mjue kuwa  mradi huu  ni mkopo  ambao utalipwa  na  watanzania  wote  hivyo nawakumbusha  kutumia  fedha  hizi katika shughuli  zilizokusudiwa  kwa  uangalifu  ili  yapatikane manufaa yaliyotarajiwa  na  serikali  haitakubali kuona  mtu ama taasisi  ikikwamisha  mradi  huu”

  Alisema  taasisi  zote  zinazohusika  ,sekretarieti  za mikoa ,Halmashauri  za wilaya  na  vijiji  kutoa  ushirikiano  wa kutosha  wa kufanikisha  utekelezaji wa  shughuli  za  mradi  huo  ikiwa ni pamoja na kuhakikisha  sheria  zinafuatwa na  hakuna  uvamizi  wa shughuli za  kibinadamu  katika  vyanzo vya maji  na  hifadhi .

Akielezea   kuhusu  changamoto na migogoro  kwa wananchi wanaozunguka   hifadhi aliagiza  kikosi kazi   kuhakikisha   kinapitia upya mipango ya  matumizi ya  ardhi  kwa  kuhusisha  baadhi ya  sheria au kutunga upya  sheria .

“ Kwa  upande wa  wananchi  nafahamu   kuwa kwa  muda mrefu  mmekuwa mkitumia  mazao ya   hifadhi  hizi  kujikimu ila  niwaambe sasa  muda  umefika  wa  nyinyi  kuchangamkia  fursa  mbadala za kiuchumi  zitakazoletwa na  mradi wa REGROW  kwa  uongozi  wa mikoa  ni  vema   mkatoa elimu  kwa  wananchi wa  mikoa yenu ili  wananchi waweze  kuzichangamkia na  kujiepusha  na vitendo vya uharibifu  wa raslimali  misitu na wanyamapori”

Pia  alisema  ujenzi wa mageti ya  kisasa  kwenye hifadhi  yatasaidia  ikiwa  mradi huo  utatanuliwa na  kuhakikisha kuwa   mipaka  hii haiwekwi tu  kwenye hifadhi  bali   pia  kwenye  maeneo oevu yote  na ili  kuhakikisha  mradi   unakuwa na tija  taasisi  ya  NEMC  chini ya ofisi ya makamu wa Rais  inategemewa kuharakisha  tathimini ya mazingira ya  bonde  la  Ruaha  ili  kuhakikisha kuwa  mradi  utanuzi wake unatekelezwa  kwa ufanisi  bila  athari  zozote za mazingira  baadae .

Kwa  upande  wake   waziri  wa maliasili na  utalii Dkt  Hamis  Kigwangala pamoja na  kutumia mradi huo kutuma salam  kwa  majangili  kuwa sasa  watabanwa  popote  walipo na hatakubali kuona  ujangili  ukiendelea  katika   hifadhi hapa  nchini  bado  aliipongeza benki ya  dunia  kwa  kuikopesha  Tanzania   wa dola za kimarekani  milioni 150 .

Kuwa mradi huo utatekelezwa kwa  miaka 6 lengo la mradi ni kukuza utalii na  kipato  cha wananchi kwa  kuboresha miundombinu  ,kujenga uwezo katika usimamizi wa  maliasili na  kuwezesha  wananchi  wanaozunguka  hifadhi  kuzalisha kwa tija.

Alisema  mradi wa Regrow  utaanza kutekelezwa  katika  hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha ,mikumi , Udzungwa  na  pori la akiba la  Selous (kanda ya  kasikazini ya  Soleus kunakofanyika  utalii wa  picha”

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE