February 2, 2018

ACHENI KUONGEZA MAUMBILE-SERIKALI

Na Katuma Masamba, Dodoma
Serikal imewataka watu wanaotumia dawa za kuongeza maumbile kuacha kutumia dawa hizo kwa kuwa madhara yake ni makubwa ikiwemo kusababisha saratani kwa watumiaje wake.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo aliyetaka kujua kama dawa za kuongeza maumbile zina athari kiafya na tamko la serikali kuhusu dawa hizo.

“Mwenyezi Mungu alituumba kila mtu kwa aina yake na rangi yake na maumbile yake, nyongeza hizi kitaalamu zina madhara kama vilivyo vipodozi haramu, ngozi ina matumizi yke Mwenyezi Mungu hakuiweka kimakosa, inatusadia sisi kujikinga na mionzi na magonjwa, matumizi ya vipodozi moja yanaleta madhara katika ngoz lakini pili vinaweza kuleta saratani,” amesema Ndugulile.

Amewataka wananchi kuacha kutumia vipodozi na dawa za kuongeza maumbile kwa kuwa madhara yake ni makubwa na gharama za kujitibu ni kubwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE