January 28, 2018

ZUIO LA MIKUTANO YA KISIASA LIMEONGEZA UTENDAJI KWA WABUNGE MAJIMBONI - PROF MAJI MAREFU

Image result for MAJI  MAREFUZUIO la  mikutano ya  hadhara  ya  kisiasa hadi mwaka 2020 lililotolewa na Rais Dkt John Magufuli  kwa wanasiasa nchini linaongeza ufanisi mkubwa  kwa    kila  mbunge mwenye nia ya  kweli  kuwatumikia  wananchi wake kuwajibika  kuwaletea maendeleo wale  waliomchagua .

Mbunge wa Korogwe Vijijini mkoani Tanga Steven Ngonyani  maarufu kwa  jina la Prof Maji Marefu ni mmoja kati ya  wabunge  wa Chama cha mapinduzi (CCM) ambae anapongeza zuio  la mikutano ya kisiasa kwa  wabunge  nje ya majimbo  yao  na  kuwa  wajibu  wa  kila mbunge ni  kumwakilisha  mwananchi aliyemchagua si vinginevyo.

“ Mheshimiwa Rais  Dkt  John Magufuli kuzuia  mikutano  na maandamano ya  kisiasa kama  ilivyokuwa  wakati  huo kabla ya  kuingia Ikulu ni  jambo la  kumpongeza  sana kwani aliona mbali  baadhi ya wabunge  hasa wa  vyama  vya  upinzani kazi  yao ilikuwa ni kuzunguka  kufanya maandamano bila kuwatumikia  wananchi waliowachagua”

Kuwa kuzunguka  kwa wabunge wa  upinzani muda  wote  katika majimbo mengine  si  tu kulikuwa  kuna wachelewesha  wananchi wa majimbo yao maendeleo  ila hadi  wananchi  wa majimbo hayo  waliyokuwa  wakifanya  mikutano walikuwa  wakishindwa kufanya shughuli  za  kimaendeleo  wakishiriki  siasa hizo.

“Unapo chaguliwa mbunge unatakiwa ujikite kwenye jimbo lako na kutatua kero za wananchi wako sio kwenda kwenye jimbo la mtu mwingine  kufanya mikutano na kumshambulia kisiasa hii haikuwa  sawa kabisa”

Kuwa Demokrasia  ya  kweli ni  mtu kuwa na huru kufanya chochote bila kuvunja  misingi ya sheria na katiba lakini   demokrasia hiyo hiyo unaweza ukaiharibu kama unakwenda kwenye eneo la wazi kufanya mikotano na kuwashambulia viongozi kwa matusi  kwa kuwadhalilisha hiyo sio demokrasia
kwa msingi wa sasa hivi walikuwa wanalalamika hawapewi nafasi katika serikali,walikuwa wanaishia tu katika kufundisha sasa hivi ni zamu yao nao kuwepo serikalini katika nyanja mbalimbali


katika nafasi za uongozi unapo kuwa umesomea eneo fulani na ukakabidhiwa nyazfa hivo kila kiongozi anae kuja huwa anamtazamo wake kwahiyo mtanzamo wake sio mbaya kila atakae teuliwa atakuta wazoefu wataelekezana tu kazi,ila kuna wengine walikuwa sugu hawashauriki baadhi ya watendaji sasa hao ndio shida


mashamba mengi baadhi yao yalikuwa yamerudishwa mengine yalikuwa bado waziri mwenye zamana ya ardhi alikuja na aka yahakiki yote na sasa hivi yapo mezani ya raisi kwa ajili ya kuyatolea maamuzi


sasa hivi mohammed ameleta vifaa vya kutosha na ameanza kuvunja mapori na kupanda mkonge mpya kwa hiyo kwa upande wake nimeona jitihada zinaonekana


nilitoa maamuzi kwenye vyombo vya habari kwamba tutalilinda wenyewe lkn haitapendeza kama mwananchi watakosa kazi badala yake walete watu kutoka kenya kuja kufanya kazi haitapendeza na hatutokubali

 

kero ya maji nina tarafa 4,nina kata 29,nina vijiji 118,na vitongoji 610 katika mradi wa benki ya dunia,nilipata maji katika vijiji kumi katika tarafa zote 4,alafu nikaomba msaada kwa UNDP wakanipa fedha nikachimba napo visima virefu 11 katika sehemu tofauti tofauti na bado nina mradi mkubwa wa maji unao toka mkoa kilimanjaro unakuja mpaka kwenye jimbo langu,alafu ofisi ya makamu Raisi mazingira walinisambazia maji kwenye vijini 15,lakini bado tunachangamoto kubwa sana ya maji kutokana na ukubwa wa jimbo langu!


nakwenda na agenda tatu,agenda ya kwanza ni Rea,agenda ya pili vituo vya afya,agenda nyingine ni Ardhi nitalisemea katika bunge linalo kuja


tumeboresha vituo vya afya kwa kukarabati vituo vya mombo,bungu magoma,na vilevile kujenga kituo cha afya kikubwa katika tarafa ya mombo kata ya mkumbara alafi vile vile tumeboresha elimu kwa kujenga high school katika tarafa  ya bungu,magoma,mnyuzi, na vile vile tumezijenga upya shule za msingi katika jimbo langu na hela chache tumetumia kwa kujenga madarasa mengi kwa hela chache,korogwe imekuwa ya mfano kwa wilaya mbalimbali kuja kujifunza matumizi ya fedha

kwa upande wa kilimo kufatana na uhaba wa ardhi wananchi wameingia sana mabondeni na kupa nda mpunga kilimo cha umwagiliaji;barabara tumejaribu kuzirekebisha ili zipitike wakati wote;nimeamua bila kutumia hela ya serikali wala ya mfuko wa jimbo kufyatua tofali elf 20 na kugawa kwa wananchi kwenye vijiji vyao walio jitolea nguvu zao wenyewe na kuweka msingi mm nawapa tofali;kwa shule natoa tofali 650,kwa zahanati natoa elf moja na hamsini,ofisi ya serikali ya kijiji natoa tofali mia tano bila mkono wa serikali


mfuko wa jimbo 2017---2018 nimegawa kama kama ifutayo kata makuyuni sh 2000000 kata ya mlungui3000000  kata ya lewa sh2000000 kata foroforo 2000000 kata ya vugiri 3500000 kata dindira2000000 kata magira gereza 2000000 kata kalalani2000000 kata ya mswaha 20000000 kata mashewa 2000000 kata ya kwagunda2000000 kata ya chekelei2000000 kata kwalukonge 2000000 kata kwashemshi 2000000 kata mkomazi 1000000 kata bungu

Bungu 3000000 kerenge 2000000 mnyuzi 1000000 mombo 2000000 naomba baadaye nitume picha na maelezo ya ziada asanteni


Vikundi ya vijana na kina mama kila vikundi vina asilimi 5 wanapewa ili waendeleze mirandi ilioanzishwa  ila wilaya yangu inasua sua sana kwa vyanzo vya mapato

Ushauri nazingatia nikienda kwenye mikutano ya hadhara nitalisemea na wenyewe wakiwepo mafisa mifugo

 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE