January 1, 2018

WATU 2 WAUWAWA KATIKA MAANDAMANO NCHINI KONGO

Image result for WATU 2 WAUWAWA KATIKA MAANDAMANO NCHINI KONGO

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema maafisa wa usalama wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewapiga risasi na kuwauwa watu wawili wakati wa maandamano ya kumpinga rais Joseph Kabila katika jiji la Kinshasa.
Mkurugenzi wa Afrika ya Kati wa Human Rights Watch Ida Sawyer amesema watu hao wameuliwa nje ya kanisa la Mtakatifu Alphonse katika wilaya ya Matete huko Kinshasa.
 Msemaji wa polisi Pierrot Mwanamputu amekanusha kwamba polisi wametumia risasi wakati wa maandamano hayo.
Wanaharakati wa Kanisa Katoliki ndio walioitisha maandamano hayo baada ya misa ya Jumapili kupinga mageuzi ya katiba yatakayo mpa nafasi rais Kabila kuwania muhula mwengine katika uchaguzi utakaofanyika mwishoni mwa mwaka ujao wa 2018.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE