January 1, 2018

WATALII 10 RAIA WA MAREKANI WAFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE COSTA RICA

Image result for WATALII 10 RAIA WA MAREKANI WAFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE COSTA RICA
Watu 12 wamefariki  kwenye ajali ya ndege magharibi mwa Costa Rica.
Kumi kati ya wale waliouwa walikuwa ni raia wa Marekani akiwemo rubani raia wa Costa Rica na rubani msaidizi.
Vyombo vya habari vilisema kuwa watano kati ya wale waliouawa walitoka familia moja.
Ripoti zinasema kuwa ndege hiyo ya injini moja ya Cessna 208 Caravan, ilikuwa safarini kutoka mji mkuu San José kwenda Punta Islita ambalo ni eneo la kistarehe.
Hukukuwa na manusura na wala haibainiki ni nini kilisababisha ajali hiyo.
Kisa hicho kilitokea katika eneo la milima karibu na Bejuco mkoa wa Guanacaste
Rais wa Costa Rica alithibitisha ajali hiyo katika taarifa iliyochapishwa mitandaoni akisema kuwa serikali yake imesikitishwa sana na vifo hivyo.
Mtangulizi wake rais wa zamani Laura Chinchilla, aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa mmoja wa wahudumuwa marubani alikuwa na binamu wake.
map


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE