Rais wa Palestina Mahmoud Abbas
anasema kuwa hawezi kamwe kukubali mpango wowote wa amani wa Marekani kufuatia
hatua hiyo ya Trump.
Maandamano yalizuka katika ukanda wa Gaza baada ya tangazo hilo.
Azimio la Umoja wa Mataifa la kuitaka Marekani kufuta tangazo
hilo lake liliunga mkono kwa wingi na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Wapalestina 13 wameuawa kwenye ghasia kufuatia tangazo hilo la
Trump wengi wakiuawa wakati wa makabiliano na wanajeshi wa Israel.
Mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na
wapalestina.
Israel ilitwaa eneo la mashariki mwa mji, ambalo awali likuwa
linakaliwa na Jordan wakati wa vita vya mwaka 1967 vya masahariki ya kati na
inadai kuwa mji huo wote ni wake.
Jana Jumapili Bw Abbas aliutaja Jerusalem kuwa mji mkuu wa kiroho
wa watu wa Palestina.
Jurusalem kuwa mji mkuu wa Israel ni hatua ambayo haijatambuliwa
kimataifa, na nchi zote zimeweka balozi zao huko Tel Aviv.
Hata hiyo Rais Trump ameiambia wizara ya mashauri ya nchi kigeni
kuanza mchakato wa kuhamisha ubalozi wa Marekani kwenda Jerusalem.
Wapalestina wametangaza kuwa wamemuita balozi wao kutoka nchini
Marekani kwa mazungumzo, wiki kadhaa baada ya rais Donald Trump kutambua
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE