January 15, 2018

WANASHERIA:TUNAMPELEKA LISSU MAHAKAMANI


Mwenyekiti wa CZI Company, Cyprian Musiba amesema kuwa yeye pamoja na baadhi ya wanasheria wamekusudia kumfikisha mahakamani Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kutokana na kauli zake alizotoa wiki mbili zilizopita akiwa nchini Kenya. 
Musiba amesema hayo leo January 15, 2018 akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa Tundu Lissu ameichafua nchi kitaifa na kimataifa kwa kauli zake kuwa Tanzania siyo nchi ya amani, na kudai kuwa Tundu Lisssu amesema uongo kuhusu watu kuuawa hovyo.
"Tundu Lissu aliutangazia Umma na dunia nzima kwamba Tanzania sasa si salama tena, nchi hii watu wanakufa hovyo hovyo kitu ambacho si cha kweli anapotosha ila Tanzania ni salama watu wanaabudu vizuri, wanajieleza vizuri ndiyo maana mimi nipo hapa najieleza kama kusingekuwa na uhuru wa kujieleza mimi nisingekuwa hapa. Tunampeleka mahakamani kwa sababu ameidhalilisha nchi yetu Kimataifa na Kitaifa na tunampa siku mbili tu atoe ushahidi wake na uthibitisho kwamba Tanzania siyo salama" alisema Musiba
Mbali na hilo Musiba amesema kuwa matatizo yaliyopo nchini sasa hayajaletwa na Serikali ya awamu ya tano kwani yalikuwepo toka serikali zilizopita na kudai kuwa kauli ya Tundu Lissu kuwa nchi si salama yeye kama mwananchi wa kawaida ilimkera sana na kudai kama hatatoa ushaidi huo ndani ya siku mbili watampeleka mahakamani.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE