January 7, 2018

WANAKILOLO WAITAKIWA KURUDI KILOLO KUWEKEZA , DC ATAKA KILA NYUMBA KUFUNGA NYUKI

mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah akizungumza na  wananchi wa  Kilolo  waishio  jijini  Dar es Salaam  leo
Wana Kilolo  waishio  Dar  wakiwa  katika  kikao  cha  maendeleo na viongozi  wa  Kilolo  leo
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo akifurahia  jambo  leo
Picha  za matukio ya  wana Kilolo waishio  Dar 


Akizungumza  leo  katika kikao cha  pamoja  kilichofanyika   Magomeni  jijini  Dar  es Salaam  mkuu  wa   wilaya ya  Kilolo Asia  Abdalah alisema  kuwa  wilaya  hiyo  imepiga hatua  kubwa  katika  sekta  mbali  mbali  zikiwemo  za  viwanda  ,Afya  ,Kilimo  ,elimu  na  sekta  nyingine  nyingi na  hivyo kuna haja  ya  wanaKilolo  kuwa  wa  kwanza  kufika  kuwekeza  zaidi  katika  wilaya  hiyo .

“ Tumefanikiwa  kupiga  hatua  kubwa katika  sekta  mbali mbali  kama  hili  la  viwanda  tayari  Kilolo  tunaviwanda  vimeanza  vikiwemo  vya  nyanya  na  viwanda   vingine   huku  kiwanda  cha  Chai Kidabaga  kipo  mbioni  kufufuliwa “

Pia  alisema  kwa  upande  wa utalii  wilaya ya  Kilolo  imebarikiwa na  kuwa na  vivutio  vingine  vya  utalii  ila  shida  iliyopo  ni  kukosekana  kwa  hoteli  za  kitalii na  hivyo  kupitia  kikao  hicho  iwe  fursa  kwa  wanaKilolo  waishio  Dar  es Salaam  na  nje  ya  Kilolo  kufika  kuwekeza  katika  sekta  ya  utalii .

  Toka  nimefika  Kilolo  nimekuwa  nikitembelea  vivutio  mbali mbali  vya  utalii  kweli  tunavyo vingi na  vizuri   sana  naombeni sana  turudi  kuwekeza  nyumbani   ili  muweze  kuwekeza  katika   sekta  hii ya  utalii “
Mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema  kuwa  mafanikio  mbali mbali ya  kimaendeleo katika  wilaya  hiyo yamekuwa  yakipatiokana  kutokana na  ushirikiano   kati yake  mbunge  na  mkurugenzi  pamoja na  wananchi  wa  wilaya   ya  Kilolo.

Kwani  alisema  katika  kuifanya  ofisi  yake  kuwa  ni ofisi  rafiki  kwa  wananchi  ametoa  ruksa  kwa  mwananchi  yeyote  mwenye uhitaji  wa  kuonana  na  mkuu  wa  wilaya  kufika  ofisini  kwake  wakati  wowote  ila  kwa  kufikisha  mambo ya  kimaendeleo na sio  majungu  kwani  ofisi yake  haipokei  majungu .

Kwa  upande  wake  mbunge  wa  Kilolo  Venance  Mwamoto   akielezea  utekelezaji  wa   Ilani  katika  wilaya  ya  Kilolo  alisema  kuwa  wamefanikiwa  kufanya  vizuri  katika  elimu na kuwa  wilaya   hiyo  ilikuwa  nyuma  zaidi katika  elimu  ila  sasa  ndio  wilaya  inayoongoza  kwa  ufaulishaji wa wanafunzi  wa  kidato  cha  sita .

Kuhusu  sekta ya  maji  alisema  upo mradi  mkubwa  wa  maji  Ilula  unaendelea  kujengwa   pia kila kata kuna  mradi  wa  maji unajengwa  wakati  umeme  kwa kata  zote  zitapata  mwaka  huu isipo  kuwa  katika kata  mbili  pekee.

Mkurugenzi   mtendaji  wa  Halmashauri  ya  Kilolo Aloyce Kwezi  aliwataka   wana  Kilolo  kucjhangamkia  fursa  zilizopo  katika  wilaya  hiyo  na kuwa  tayari  viwanja  kwa   ajili ya  ujenzi  wa viwanda   vimepimwa .

Mkurugenzi   huyo  alisema  kuwa  wilaya  ya  Kilolo  ni  moja  ya  wilaya  ambayo  zao  la Parachichi na Korosho  zinakubali  na   hivyo  ni lazima  wananchi  hasa  wanaoishi  nchi ya  Kilolo  kurudi  kuwekeza  katika  kilimo  hicho.

Mdau   wa maendeleo  Danford  Mbilinyi  ambae  pia  ni  mkurugenzi  wa Umoja Switch alisema alisema  ni  jambo la  kushangaza  sana kuona  kijana wa  Kilolo  analalamika  kukosa  pesa  wakati kuna  ardhi  inayofaa  zaidi  kwa  kilimo  cha  miti  na hivyo  wanayo nafasi ya  kulima  miti  ambayo  itawasaidia  kiuchumi .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE