January 17, 2018

Viongozi wa Palestina watoa wito wa kutoitambua Israel kwa muda

Image result for Palestina
Chombo cha juu cha pili cha maamuzi katika Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO kimetoa wito wa kusisitisha kuitambua Israel hadi pale nayo itakapoitambua rasmi Palestina, katika uamuzi unaoweza kuyageuza juu chini mahusiano ya zaidi ya miaka 25 kati ya serikali hizo mbili. 
Taarifa iliyotolewa jana na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya chama cha PLO Salim Zanoun, imeitolea wito Kamati ya Utendaji kutoitambua Israel hadi nayo itakapoitambua rasmi Palestina, kusitisha ujenzi wa makaazi ya walowezi kwenye ardhi ya Palestina, na kufuta uamuzi wake wa kuitwaa Jerusalem Mashariki. 
Haijulikani kama Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas atatii wito wa Kamati Kuu ya chama, kwa vile alipuuza matakwa yao ya kufuta ushirikiano wa kiusalama na Israel mwaka 2015. 
Chama cha PLO kilikuwa kikikutana mjini Ramallah kutangaza mkakati wao, kufuatia hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE