January 1, 2018

VIONGOZI WA DINI WATOA NENO

VIONGOZI  wa  dini ya kikristo  mkoa  wa  Iringa  wakiongozwa na  askofu  wa  kanisa la  kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT) dayosisi ya  Iringa  mchungaji  Blaston  Gavile  wasema   Taifa  linakabiliwa  na matatizo makubwa yanayosababishwa na  uvunjifu wa  maadili  na  hivyo  kuna haja ya kuandamana  kumlilia  Mungu  juu  ya hali  ya  mambo  inayoendelea  kulikumba Taifa  la Tanzania .
Huku   serikali ya  mkoa  ya  mkoa wa Iringa ikiwataka  viongozi wa  dini kuacha kutumia  lugha  zisizo faa kwa Rais Dkt John Magufuli na kumtaka askofu  Zacharia Kakobe pesa  zake  nyingi alizokuwa nazo kusaidia  mkoa  wa Iringa ambao  unahitaji  pesa za maendeleo.
Askofu Gavile  ambae   alikuwa ni  mwenyekiti wa mkesha  wa  kuliombea  Taifa  na  kuukaribisha mwaka  2018   uliofanyika  katika  uwanja  wa  Samora   juzi  alisema    kuwa  Mungu  amebariki Taifa  kuwa na raslimali mbali mbali  kama  ardhi ,madini , hifadhi  za  wanyama  ,gesi na mafuta   na nyingine  nyingi  ila tatizo  kubwa  nchini  haikuwa  na uongozi   bora  isipo  kuwa  uhalifu  uliibuka  baada ya kuporomoka  kwa maadili  miongoni mwa  viongozi   na jamii .
  Kutokana na  kukosekana kwa maadili   Taifa limekuwa  likikumbwa na magonjwa ,matendo  ya  ukatili dhidi ya   watoto ,wanawake ,imani  za kishirikina  zinazoishia  kwenye mauwaji  ya vikongwe ubakaji wa  watoto  wadogo  na  watu wenye  ulemavu  wa  ngozi  (albino)  tunamuombea  sana  Rais wetu Dkt  John Magufuli asirudi  nyuma  na aendelee kwa  kasi  hiyo  hiyo  kulirejesha  Taifa  katika  misingi  yake na kazi kubwa ya  watanzani kwa  dini  zao kuendelea  kumuombea”
Alisema  katika  kufanikisha Taifa  kuwa katika misingi  mizuri   waumini  wa dini  zote   lazima  kuwa na  mshikamano  katika mambo  muhimu  ikiwezekana  kufanya  tathimini ya mwaka  uliopita  ili kujua  ni  wapi  pa  kujipanga  mwaka  huu  vizuri  na kuwe  na tija katika  kuliletea  Taifa maendeleo .
“ Tunaamini  kwamba  ni  wajibu wa  kila  Raia   mwema  wa Tanzania  bila  kujali  kwamba  ni  mwanaume ama  mwanamke ,mzee  ama  kijana  iwe  ulipiga kura  ama hukupiga kura   lakini  unaona  kwamba  unadaiwa  kushiriki na  kuomba  ili  kuleta  badiliko chanya  katika  Taifa  letu   Mungu anatafuta  mtu  atakayesimama  katika  nafasi  iliyowazi  kwa  niaba ya  nchi yetu”
Hivyo  alisema  viongozi wa  dini  ni  chachu  nguzo  na taa  ya umoja  ,maovu mengi  ya  jamii  isiyo  faa  ni matokeo ya sauti  mbali mbali  za  viongozi  wa  dini wanao kinzana  lazima  viongozi wa  dini  kusimama vizuri  kama  viongozi  wa  dini  na  sauti ya  Mungu kwa  nchi ya  Tanzania  hivyo  suala  la  kuendelea  kuwa na mikusanyiko kwa ajili ya  kuwaandaa viongozi   na  watu ambao wanalibeba  Taifa  ni  suala la  msingi .
Askofu Gavile alisema  wao kama  viongozi  wa  dini  wanatambua  kazi kubwa  inayofanywa na  serikali ya  awamu ya  tano  ya kusimamia  na  kupigania rasilimali  za Taifa  la Tanzania  na  wanatoa  pongezi nyingi  kwa  serikali hasa  Rais na  wasaidizi wake   wote .

  TUnahitaji  ushindani  bila  kujali  itikadi  za  vyama  vya  kisiasa  tushirikiane bila  kutumia  maneno  magumu  yanayo hatarisha  amani  na  upendo  na mshikamano tulionao  Kitaifa  ambayo ndiyo  Tunu  muhimu  kwa  nchi  yetu tupinge kwa  nguvu zetu zote  kushiriki matendo   maovu yanayoweza kuvunja amani yetu  pia  tuendelee  kuombea hali ya huduma  za afya katika mkoa wetu wa Iringa tunaomba  serikali  kutatua changamoto hasa za matibabu kwa  wazee,wanawake wajawazito na  watoto  ila  pia  upungufu wa madaktari na wauguzi  pamoja na upatikanaji wa  dawa  kwa wakati “
Kwa  upande   wake mgeni  rasmi katika  mkesha  huo mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  aliyewakilishwa na  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  alisema  kuwa  kuna haja ya maaskofu  kuepuka  lugha za  uchochezi  kwa jamii na  viongozi wa  juu   kwani kwa  kuendelea  kuruhusu  lugha   za  kichochezi ni kulibomoa  Taifa .
Alisema  inashangaza  sana   kusikia  askofu  akimwambia  askofu  mwenzake  akatubu na  mchungaji  kumwambia  mchungaji  mwenzake akatubu  na kuwa  lugha  za  kichochezi kama  hizo hazitavumilika  kwani  Rais  ni  kiongozi  wa  juu katika  Taifa   hili leo  anapotokea  askofu  Zacharia Kakobe  kutoa  lugha  isiyofaa kwa  Rais  ni kutomtendea  haki .

“ Rais  ni  askofu  wa nchi  hii  ,mkuu wa  mkoa ni askofu  wa  mkoa kama  ilivyo kwa  mkuu  wa  wilaya ni askofu wa  wilaya  husika  hivyo kuna  njia  ya kumshauri  ama  kushauriana  bila  kuvunjiana  heshima  na  bahati mbaya  unavyomsema  hibaya    Historia  yako  inaonyesha  ulikuwa katika  mchakato wa chama   Fulani  cha  siasa hivyo lazima jamii  itajua  ujumbe  wako ni wa kisiasa “
Hivyo  alisema  kuwa lazima  viongozi wa  dini kuepuka  kujiingiza katika  siasa na  kuifanya kazi ya  kiroho  bila  kutumika na  vyama  vya  siasa .
  Viongozi  wa  dini  tusaidieni  pia  kuwaita  kimya  kimya  viongozi wa  vyama  vya  siasa  na  kuwataka kuheshimu  Demokrasia  ndani ya  vyama  hivyo  haiwezekani  kuendelea  na  vyama  ambavyo viongozi  wake ni  wale  wale na  niwaombe  sana viongozi wa  dini tuzidi  kushirikiana na  sisi  viongozi wa  serikali  hatuna  ugomvi  wowote na  askofu Kakobe  ila  tuheshimiane  pia   nimuombe  Askofu Kakobe kama  alivyojisifia  kuwa ana pesa  nyingi  sisi hapa Iringa  tunashida ya   pesa  tunaomba atusaidie pesa”

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE