January 22, 2018

UPDATES YA KESI YA MBUNGE JOSEPH MBILINYI SUGUMBUNGE wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Jumatatu, Januari 22, 2018 kusikiliza kesi inayomkabili  ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Sugu na Masonga walifikishwa mahakamani hapo Ijumaa iliyopita Januari 19, 2018 lakini  mahakama ilizuia dhamana zao na kuwarejesha rumande hadi leo ambapo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite alitoa uamuzi huo na kwamba kesi hiyo inatakiwa isikilizwe mfululizo kwa muda mfupi huku washtakiwa wakiwa wanafika mahakamani hapo wakitokea mahabusu.

“Mahakama hii inataka kusikiliza kesi hii kwa muda mfupi sana, ndani ya wiki moja kuanzia Jumatatu ijayo (leo)  iwe imeamuriwa, hivyo washtakiwa wataendelea kuwekwa mahabusu,” amesema Mteite.

Sugu na Masonga wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo waliyatoa katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya wakati wakiwahutubia wananchi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE