January 7, 2018

TRUMP ASEMA YUKO TAYARI KUFANYA MAZUNGUMZO NA KIM

Related image
Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kiongozi wa Korea Kasazini Kim Jong Un na kuwa anatumai mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini yatakuwa na tija.
Korea Kaskazini ilikubali siku ya Ijumma kufanya mazungumzo rasmi ya ngazi ya juu na Korea Kusini wiki ijayo, hayo yakiwa mazungumzo ya kwanza kati ya nchi hizo jirani katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Akijibu maswali kutoka kwa wanahabari, Trump ameeleeza nia ya kufanya mazungumzo na Kim akisema hana shida kabisa na hilo lakini kwa masharti. Viongozi hao wawili wamekuwa wakirushiana cheche za maneno na vitisho tangu Trump alipoingia madarakani.
Trump amekuwa mara kwa mara akimuita Kiongozi wa Korea Kaskazini bwana maroketi kwa kufanyia majaribio silaha za kinyuklia na kurusha makombora, huku Kim akimuita Trump mtu aliye na akili punguani.
 Mazungumzo kati ya Korea Mbili yatajadili uwezekano wa Korea Kaskazini kushiriki mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi na uhusiano kati yao.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE