January 17, 2018

CCM MKOA WA IRINGA WALAANI TUKIO LA UVAMIZI IRINGA , ASAS AWATULIZA VIJANA UVCCM KUTOLIPA KISASI

Mwenyekiti  wa  UVCCM mkoa wa  Iringa  Kenani  Kiongosi  kulia  akimpokea  katibu  wa mkoa  Christopher Mgala  na mjumbe  wa Halmashauri  kuu ya CCM Taifa  (NEC)  Salim Asas katikati  baada ya  kufika  katika  nyumba  aliyokuwa  akiishi katibu wa  UVCCM  wilaya ya  Iringa  mjini Alophonce  Patrick Munyinga  leo
Viongozi  mbali mbali  wakimpa pole  katibu  wa UVCCM wilaya ya  Iringa  mjini Alphonce  Patrick  Munyinga  wa  pili  kulia
Katibu  wa  CCM mkoa  wa  Iringa Alphonce  Muyinga  kushoto  akipewa  pole na  katibu wa  CCM mkoa  wa  Iringa Christopher  Muyinga  leo
Mjumbe  wa Halmashauri  kuu ya  CCM Taifa  (NEC)  mkoa  wa Iringa  Salim Asas  akimpa  pole Bw  Muyinga  kushoto leo
Asas  akisalimiana na  ofisa  wa polisi  mkoa
Wananchi  wa  mjini  Iringa wakiwa  nje ya  nyumba  ya katibu  wa  UVCCM  wilaya ya  Iringa  Alphonce  Muyinga  ambayo  imeungua  moto  leo
Wahananga  wa  moto  huo
Muyinga  akiwa na  wenzake  waliokuwemo katika  nyumba  hiyo
Baadhi  ya wananchi  wakiwa  eneo la  tukio
Baadhi ya  wana vyuo  wakifika  eneo la  tukio
Mjumbe  wa  mkutano  mkuu  wa CCM Taifa  kutoka  Iringa  vijijini Arif  Abri katikati  akiwa na baadhi ya makada wa  Chadema  waliohamia  CCM
Arif  na  timu  yake  wakitazama  nyumba  iliyoungua
Hili  ndilo dirisha  ambalo  linadaiwa  kuvunjwa na  kutupiwa  kitu  chenye mlipuko
Nyavu  za  dirisha  zikiwa  zimeharibiwa 
                                      Na  MatukiodaimaBlog

CHAMA  cha  mapinduzi  (CCM)  mkoa  wa  Iringa kimelaani   matukio  ya  uvunjifu  wa  amani  yaliyoanza  kuibuka katika Manispaa ya  Iringa ndani ya  wiki   hii kwa  nyumba ya  aliyekuwa  diwani  wa Chadema kata ya  Mwangata  kuvunjwa na lile  la  kuteketezwa  kwa  moto nyumba  aliyokuwa  akiishi katibu  wa umoja  wa  vijana  wa  chama  cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya  Iringa mjini.

Akizungumza  leo  na mtandao   wa  matukiodaimablog baada ya  kutembelea  nyumba  iliyochomwa moto  katibu  wa CCM  mkoa  wa Iringa Christopher Magala alisema  kuwa   CCM  imepokea kwa masikitiko makubwa  juu ya matukio  mawili ya uharibifu  wa  nyumba  zao.

Alisema  kinachofanyika  si  siasa  ni  uharifu na  kuwa ni  vema  jeshi  la  polisi  kupambana na watu hao  wanaojihusisha na vitendo  hivyo  vya  kuharibu mali  za  wana CCM na  madiwani  wanaohama  kutoka chama  cha  Demokrasia na  maendeleo (Chadema).

Kwa  upande  wake  mjumbe  wa Halmashauri  kuu ya  Taifa (NEC)  anayewakilisha mkoa  wa Iringa Salim  Asas pamoja na  kuliomba  jeshi  la  polisi  kufanya  uchunguzi  wa  jambo hilo  alisema kuwa CCM itabeba  jukumu  zima la  kuwasaidia  wahanga  wa  tukio  hilo  pamoja na  kuwatafutia  hifadhi  ya kuishi  na mahitaji mengine  muhimu kwao .

Alisema  kuwa  tukio  hilo limekuja  ikiwa ni  siku  tatu  tu toka  nyumba ya  aliyekuwa  diwani wa kata ya  Mwangata  kupitia  Chadema  kuvunjwa na  watu hao  wasiojulikana  na  kuwa  kuendelea  kuyavumilia matukio hayo  ni  kuruhusu amani  kuvunjika .


“Kila  mmoja  wetu  ameumizwa  sana na  matukio haya   ila  nawaombeni  sana  wahanga  ondoeni  hofu  CCM itafanya  kila  liwezekanalo bila  kujali  itikadi  za  vyama  wote  mliokuwa  mkiishi katika  hii  nyumba  ambao wengi  wenu ni  wanafunzi wa chuo  kuhakikisha  mnasaidiwa  na CCM katika  hili pamoja  na  kuwa katibu  wetu  wa UVCCM alikuwa  akiishi humu ndani ila wapo wengine  hawakuwa na chama tutasaidia  jamii nzima  bila kuchagua “

Hata  hivyo  Asas  aliwataka   vijana wa  UVCCM  kutolipiza  kisasi  wala kufanya  vurugu  zozote   kwa yeyote kwani hadi  sasa kazi ya  kuwasaka  wanaohusika na matukio hayo  lifanyanywa na  jeshi la  polisi hivyo si  vizuri  kuruhusu mihemuko ya kisiasa .

“ Tunaimani kubwa na  jeshi la  polisi  litafanya kazi yake  vijana nawajua  vizuri ila  kama  chama  hatupendi kusikia  kijana  yeyote analipa  kisasa  nakuagiza  mwenyekiti  wa  UVCCM mkoa tuliza  vijana  wako “

Wakizungumza kwa nyakati  tofauti  katika eneo hilo la  tukio diwani mteule wa kata ya Kihesa  Juli  Sawani  alisema  kuwa  kuanzia  sasa  wanaanza  ulinzi  wa  sungusungu pamoja na  kuendesha zoezi la upigaji wa  kura  za  siri ili  kubaini  waharifu  kazi itakayosimamiwa na afisa  mtendaji wa kata .

Mjumbe  wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kutoka  wilaya ya  Iringa vijijini Arif Abri  akitoa  pole kwa  wahanga  hao  alisema  kuwa si vema  kwa  vyama  vya siasa kuruhusu  siasa  vya  kuvunjw

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE