January 25, 2018

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA ASASI YA MMADEA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WAUSHIRIKI WA WANANCHI KATIKA KUISIMAMIA SERIKALI (PPGO)

TAARIFA MMADEA (CMT) 25/01/2018
Mazombe Mahenge Development Association (MMADEA) ni shirika lisilokuwa la kiserikali ambalo liliundwa mwaka1999 na kusajiliwa kisheria mwaka 2000 kwa namba. SO.NO. 10300 na kupata cheti cha ukubalifu chenye namba No: 0856 mwaka 2008.

         Dira ya shirika: Kuwa  na jamii yenye maisha bora kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, manufaaa ya kijamii na kiuchumi  na ushiriki na uendelevu.
         Dhamira ya shirika:Kuiwezesha jamii kuwa na maendeleo endelevu kwa kuwajengea uwezo wa namna ya kutuza mazingira, kuboresha elimu, afya,kilimo na kuongeza kipato kwa kutumia fursa na rasilimali zilizopo katika mazingira yao,namna ya kutimiza majukumu yao na kudai haki.


         Falsafa ya shirika: MMADEA inaamini kuwa mkakati wa kimaendeleo ili kuondoa umasikini na kuboresha hali ya kijamii na kiuchumi wa jamii ya watu wa vijijini na mjini (wanawake na wanaume) ni kwa njia ya kujitegemea.

USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA KUPANGA MIPANGO YA MAENDELEO NA BAJETI YA VIJIJI KATIKA WILAYA YA KILOLO
 • Kwa ufadhili wa The Foundation for civil society (FCS) MMADEA inatekeleza mradi wa USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA KUISIMAMIA SERIKALI (PPGO)  katika wilaya ya Kilolo katika kata 4 .
1.Idete katika  vijiji vya Madege,Kiwalamo na Ilutila.
2.Ibumu katika vijiji vya Ilambo,Kilala kidewa,Kilumbwa na Ibumu.
3.Uhambingeto katika vijiji vya Uhambingeto,Kipaduka,Ikuka
4.Nyanzwa katika vijiji vya Igunda, Nyanzwa,Mgowelo
Lengo la mradi ni kuishirikisha jamii katika mifumo ya upangaji mipango na bajeti  katika sekta mbalimbali kwa kutumia dhana ya uwajibikaji jamii (SAM) hususani dhana ya fursa na vikwazo  kwa maendeleo( O&OD).
Malengo mahususi:
 1. Kuongeza ushiriki  wa jamii katika upatikanaji wa taarifa za mchakato shirikishi jamii wa upangaji mipango na bajeti katika nyanja mbalimbali mfano kilimo, elimu na maji ili waweze kushiriki kikamilifu.
 2. Kuwa na jamii yenye uelewa na inayodai uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma bora.
Matokeo tarajiwa:
 1. Kuwepo kwa mazingira wezeshi kwa jamii kushiriki kikamilifu katika mchakato shirikishi wa upangaji mipango na bajeti ya nyanja mbalimbali mfano kilimo, maji na elimu kwa kutumia dhana ya fursa na vikwazo katika maendeleo yaani O&OD.
 2. Kuwa na jamii inayodai uwajibikaji katika utekelezaji.

SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA KWA ROBO YA KWANZA(MWEZI 8 HADI 10/2017NI KAMA ZIFUATAZO:-
 1. Kufanya utambulisho wa mradi kwa halmashauri ya wilaya na wadau wa maendeleo ili kupata maoni na ushauri kuhusu mradi huu.
Walengwa
Waliofikiwa
50
50

 1. Kufanya ushawishi na utetezi kwa viongozi 390 ili waone umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika kuibua na kupanga vipaumbele vyao kwa kutumia dhana ya fursa na vikwazo kwa maendeleo kwa jamii ( O& OD).
Walengwa
Waliofikiwa
390
387


 1. Kuendesha mikutano mikuu maalumu kwa wananchi 1040  ili waweze kuona umuhimu wa wao kushirikiki kikamilifu katika kuibua na kupanga vipaumbele vyao viingizwe kwenye mpango wa maendeleo ya vijiji kwa siku moja kwa kila kijiji.
Walengwa
Waliofikiwa
1040
1745

 1. Kuendesha mikutano mikuu maalumu 13 ya uhamasishaji ili wananchi wafahamu kazi na wajibu wa maafisa ugani wa nyanza zote.
Walengwa
Waliofikiwa
1040
1822

 1. Kuendesha mafunzo/mafunzo rejea kwa viongozi wa serikali wa vijiji juu ya utawala bora, kazi na wajibu viongozi wa vijiji na maafisa ugani na maadili ya viongozi na watumishi wa umma.
Walengwa
Waliofikiwa
390
380

 1. Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mradi.
Walengwa
Waliofikiwa
100
90


SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA KWA ROBO YA PILI (MWEZI 11/2017 HADI 01/2018) NI KAMA ZIFUATAZO:-
 1. Kufanya mafunzo elekezi kwa wajumbe wa serikali za vijiji kuhusu namna ya kuandaa mipango na bajeti kwa kutumia dhana ya O&OD.
Walengwa
Waliofikiwa
390
274

 1. Kufanya mikutano mikuu maalumu ya vijiji kwa kushirikiana na wananchi katika kuandaa mipango ya maendeleo ya vijiji ya muda mrefu na mfupi kwa kutumia dhana ya O&OD.
Walengwa
Waliofikiwa
1040
2791

 1. Kushiriki katika mikutano ya maendeleo ya kata na kuona na kushauri jinsi gani vipaumbele vya wananchi vinaingizwa katika mpango wa maendeleo wa kata.
Walengwa
Waliofikiwa
80
75

 1. Kufanya mikutano maalumu ya vijiji ili kuangalia mabadiliko yaliyojitokeza baada ya kufanya mafunzo kwa jamii (viongozi na wananchi) juu ya dhana ya upangaji mipango shirikishi jamii (O&OD)
Walengwa
Waliofikiwa
1040
1789

5.      Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mradi.
Walengwa
Waliofikiwa
195
128

MAFANIKIO
 1. Vijiji vimeanza kuendesha mikutano ya vitongoji kwa lengo la kuwaelimisha umuhimu wa wao kushiriki mikutano na kukusanya maoni mfano kijiji cha Ilambo katika vitongoji vya mavigili,lugolofu,magunga na ilambo. Awali hawakuona umuhimu wa kuitisha mikutano ya kitongoji.
 2. Kuna nuru ya ushirikiano na uwajibikaji wa pamoja kati ya viongozi wa kisiasa (Madiwani), wenyeviti wa vijiji, vitongoji na watendaji baada ya kutambua mipaka yao ya uongozi ( kanuni na taratibu za uongozi) na kuacha kuwatisha viongozi wa vijiji na watendaji mfano kijiji cha Kiwalamo na Ibumu. Ambapo madiwani waliwatisha kuwafukuza kazi wenyeviti wa vijiji.
 3. Viongozi wa vitongoji wameanza kuandaa kalenda ya mikutano na kuandika mihtasari ya mikutano tofauti na awali hata wakiitisha walikuwa hawaandiki mfano vijiji vya Mgowelo, Ilambo Ikuka, Uhambingeto na Madege.
 4. Kuimarika kwa ushirikiano kati ya halmashauri (watendaji wa halmashauri), Ofisi ya mkuu wa wilaya, MMADEA na wananchi katika kutekeleza miradi.
         Wananchi wanadai mikutano ya uelimishaji ya mara kwa mara kutoka halmashauri na MMADEA baada ya kugundua baadhi ya viongozi hawapendi kuitisha mikutano (mfano kata ya Idete).
         Ofisi ya mkuu wa wilaya imeahidi kushiriki katika mradi kwa kufuatilia utekelezaji kwenye halmashauri ya wilaya  na wananchi.
       Hivyo kuna dalili ya umiliki wa mradi hata baada ya mradi kumalizika.
5.    Viongozi wametambua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika kutambua matatizo yao na kujitegemea wenyewe kuliko kusubiria ahadi za viongozi wa ngazi za juu.
            Kwa mfano:- Kubuni miradi iliyo ndani ya uwezo wao kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuikamilisha (mfano kijiji cha Mgowelo – zahanati).
6. Mapokeo ya mafunzo yamekuwa chanya na jamii (viongozi na wananchi) wameelewa zaidi namna ya kuandaa mipango na bajeti inayozingatia fursa walizonazo. Mipango ya maendeleo iliyowasilishwa haikuwa tegemezi kwa kiasi kikubwa. Hivyo wananchi wameelewa umuhimu wa kuanzisha na kumaliza miradi kwa kutegemea jitihada jamii.
7. Dhana ya upangaji mipango shirikishi jamii imeanza kuzingatiwa , mfano ushirikishwaji katika ngazi ya kitongoji, kutambua fursa na  uzingatiaji wa vipaumbele katika sekta ya maji, kilimo,afya na elimu.
8. Wajumbe katika mikutano mikuu ya vijiji na  KAMAKA  walishiriki kikamilifu katika kuibua kujadili na kufanya marekebisho ya mipango na kupitisha mipango ya maendeleo ya vijiji na kata ambayo iligusa sekta zote muhimu kama  vile Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Mazingira, michezo na gharama za uendeshaji wa ofisi.
9. Ushiriki wa wanawake katika mikutano na kuchangia kwenye mikutano hiyo umeongezeka. Mfano kijiji cha Mgowelo, Kilumbwa, Uhambingeto, Ilutila na Ilambo.
10. Uwepo wa maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya wilaya katika utekelezaji wa mradi huu imesaidia sana kutatua baadhi ya kero za muda mrefu sana za wananchi.

TULICHOJIFUNZA
         Wanawake wakishirikishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo wana michango mingi yenye tija kwa maendeleo ya jamii.
         Kuna haja ya watendaji wapya kupata mafunzo elekezi ya namna ya ufanyaji kazi.
         Viongozi na watendaji wa vijiji wanachangia kufifisha ushiriki wa wananchi katika kupanga mipango na bajeti.
         Kuna haja kubwa ya kuwaelimisha mara kwa mara wananchi na viongozi wao juu matumizi sahihi ya rasilimali zinazowazunguka katika kutekeleza miradi kwani wao wana utayari katika kutekeleza baadhi ya miradi ndiyo maana walitaka kufahamu taratibu za uvunaji wa Misitu ili waweze kutumia na kufanikiwa na rasilimali hizo.

         Wananchi wakishiriki na kushirikishwa kwenye kuibua, kujadili na kuipitisha miradi kuna uhakika kwa miradi hiyo kutekelezwa kwa asilimia kubwa kwani watakuwa wameimiliki na hivyo kurahisisha uchangiaji wa mali na nguvu kazi pasipo kutegemea misaada mbali mbali kutoka nje na kutumia fursa zinazowazunguka.

         Ushiriki wa wanawake kwenye mikutano haukuwa wa kuridhisha sana ingawa umeboreka kulingana na awali.

         Kuna ufahamu mdogo wa namna ya kuandika mihutasari katika ngazi za vitongoji na vijiji. Elimu zaidi inahitajika.

         Kushiriki kwa wananchi katika kuibua changamoto na kupanga vipaumbele kumesababisha maeneo au changamoto zilizokuwa hazipewi kipaumbele kuibuliwa hasa na makundi ya wanawake.

         Msaada wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa Halmashauri bado unahitajika kwa kiasi kikubwa ili kuwezesha miradi ya vijijini kutekelezwa kwa ufanisi (mfano masuala ya majengo).

CHANGAMOTO
 1. Baadhi ya watendaji wa kata na vijiji kuchelewesha taarifa za mikutano kwa viongozi wa vijiji na wananchi kwa sababu zilizo nje ya utendaji wao wa kazi (mfano kata ya Ibumu na Idete.)
Utatuzi:Hali hiyo ilirekebishwa katika ufuatiliaji wa ufikaji wa taarifa kwa walengwa (wananchi).
       :Pia wameelimishwa kukasimisha madaraka pale wawapo na dharura au majukumu mengine.

2. Ukubwa wa vijiji ambapo vitongoji viko mbali sana na ofisi za vijiji au kata hali inayopelekea wananchi kufika kwa kuchelewa na wakati mwingine kutohudhuria .

Utatuzi:Walisubiriwa. Pia ilishauriwa mikutano iwe inazunguka kwenye vitongoji ili wananchi wote waweze kufikiwa.
3.Wanasiasa na wananchi kuingiza ajenda zao kwenye mikutano hali inayoyumbisha mwenendo lengwa wa mkutano.

Utatuzi: walielimishwa wawe wanaitisha mikutano ya mara kwa mara.
        :wananchi waliombwa wawe na subira na wawe wanahudhuria mikutano ili waweze kujadili na kupata ufafanuzi wa kero hizo pindi mikutano inapoitishwa na viongozi wao.

4. Kupata ushirikiano hafifu kutoka kwa mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Kilala kidewa.
Utatuzi: tulishirikiana na diwani na wajumbe wa serikali ya kijiji kuendesha shughuli za mradi.

YALIYOJITOKEZA WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MRADI
       Wananchi wanadai kwamba hawatembelewi na
viongozi (wabunge, DC na madiwani) na watendaji ngazi za Halmashauri ya wilaya na kata – maafisa maendeleo ya jamii, mipango na maafisa ugani.

Viongozi na wananchi wanadai kuelekezwa taratibu za kutumia rasilimali zinazowazunguka kama vile misitu, mawe na maji kwenye miradi ya vijiji vyao.

       Wananchi wanadai wamesahaulika kupatiwa watendaji kwa mfano kijiji cha Madege toka kilipoanzishwa hakijawahi kuwana afisa mtendaji wa kijiji. Pia kata ya Uhambingeto hawana afisa maendeleo ya jamii.

       Viongozi wa kijiji hawafuatiliwi kwa karibu kunakopelekea viongozi hao kufanya kazi kwa mazoea. Kwa mfano afisa mtendaji na mwenyekiti wa kijiji cha Kilala kidewa wanafanya kazi kwa kuvunja taratibu za ofisi jambo ambalo linaonyesha hawajui wajibu wao.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE