January 25, 2018

TAARIFA TOKA TAASISI YA ISICO KWA UMMA JUU YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA HAKI SAWA YA UMILIKI WA ARDHI KWA WANAWAKE NA WASICHANA WILLAYA YA KILOLO


IRINGA CIVIL SOCIETY ORGANIZATIONS

[ICISO- UMBRELLA]

BOX 317, Iringa Tanzania Email. iciso@yahoo.com

Mobile: 0753663282, 0764717181, 0754 768768, 0754 645670.MUHTASARI WA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO.


Iringa Civil Society Organization (ICISO-UMBRELLA) ni mwavuli wa asasi za kiraia katika mkoa wa Iringa ambao umesajiliwa mwaka 2001 kwa namba SO.NO.10966 na kupata cheti cha ukubalifu (compliance certificate) mwaka 2013 chenye namba 00001548 ili kuendana na sheria ya NGOs namba 24 ya mwaka 2002. Ofisi zetu zinapatikana kata ya Mtwivila, Mtaa wa Mtwivila B katika Manispaa ya Iringa.

ICISO imefanya kazi katika mkoa wa  Iringa tangu mwaka 2002 hadi sasa katika nyanja za afya, mazingira, elimu, utawala bora na kilimo.Baadhi ya shughuli tulizofanya ni kama vile za TB, afya, mabadiliko ya tabianchi, kilimo na umwagiliaji, midahalo mbalimbali ya amani, usawa wa kijinsia, utawala bora, mabadiliko ya tabianchi, kukutanisha wawakilishi wa wananchi na wananchi majimboni.


Wilaya ya Kilolo.

  1. Image (Image, Iyai, Uhominyi, Ilawa na Lyasa).
  2. Kising’a (Kisinga, Barabara Mbili, Kidumka na Isele)
  3. Ukumbi (Ukumbi, Winome na Kitowo)
  4. Mahenge (Mahenge, Irindi na Magana)


Lengo la mradi ni:-

 Kuboresha mazingira ya upatikanaji wa ardhi na haki nyingine za umiliki wa mali hasa kwa wanawake na wasichana katika wilaya za Iringa na Kilolo.

Malengo mahususi:

      Kuimarisha uwezo wa wanawake na wasichana kuwa na haki sawa katika kupata, kutumia na kumiliki ardhi.

      Kuboresha mazingira kwa makundi yaliyotengwa (wanawake na wasichana) kwa kutumia serikali na vyombo vilivyoundwa (kamati za vijiji na mabaraza ya ardhi ya kata) ili kuwawezesha kupata na kutumia ardhi na mali nyingine.

      Kuimarisha uwezo wa vijiji kuwa na kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi.


SHUGHULI ZILIZOPANGWA KUTEKELEZWA KWA ROBO YA KWANZA.

1. Kufanya utambulisho wa mradi kwa Halmashauri ya Wilaya na wadau wa maendeleo ili kupata maoni na ushauri kuhusu mradi huu wajumbe 20.

Jumla ya washiriki 20 kutoka halmashauri, na serikali za vijiji walishiriki wakati wa kutambulisha mradi.

2. Kufanya utafiti ili kujua halihalisi ya sasa na Kutoa taarifa kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya, vijiji kata na wadau mbalimbali kwa wananchi 180. Jumla ya wananchi na viongozi 177 walifikiwa wakati wa baaseline survey.

3. Kuendesha mafunzo kwa viongozi wa serikali za Vijiji, kamati za ardhi za Vijiji na mabaraza ya kata kwa viongozi 100. Viongozi 91 wa vijiji walifikiwa na kupata mafunzo

4. Kuanzisha, kutoa mafunzo kwa vikundi vya ngoma vya kijamii juu ya umuhimu wa wa wanawake kumiliki ardhi na mali nyinginezo kwa kila kijiji.

Vikundi 15 vimepewa mafunzo juu ya umuhimu wa wanawake kumiliki ardhi na mali nyinginezo na wameanza kutunga nyimbo za kuhamasisha jamii kumiliki ardhi na mali nyinginezo. (See Video)

5. Kuendesha mikutano 15 ya hadhara kwenye vijiji vyote vya mradi.

Tulifanikiwa kufanya mikutano katika vijiji 15 na kudhuriwa na wananchi jumla ya 1480.

6. Kuendesha mikutano 4 na Kamati ya Maendeleo ya Kata (KAMAKA) kwa ajili ya kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi na kujadili njia wezeshi za kumwezesha mwanamke kumiliki ardhi.  Wajumbe 55 walifikiwa

7. Kuendesha midahalo 4 ya wanawake na wasichana, viongozi wa mabaraza ya ardhi, Azaki na wadau wengineo juu ya mila kandamizi dhidi ya wanawake kupata haki ya kumiliki ardhi na mali nyinginezo kwa kila kata wajumbe 30.

8. Kuendesha midahalo 4 juu ya kutoa fursa kwa wanawake na wasichana kujadili na kueleza changamoto/kero wanazokabiliana nazo katika suala la umiliki wa mali na ardhi wanapopeleka kero/malalamiko yao kwenye vyombo vilivyopewa mamlaka katika maeneo yao, na nini mapendekezo yao.

8. Kuendesha vipindi vya redio.

9. Kufanya tathmini na ufuatiliaji.

MAMBO TULIYOJIFUNZA.

Ø  Idadi kubwa ya wanchi hawana uelewa juu ya haki sawa ya kupata, kutumia na kumiliki ardhi.

Ø  Bado kuna haja ya kuendelea kutoa mafunzo na kuhamasisha jamii juu ya usawa katika umiliki wa mali na ardhi katika jamii.

Ø  Mwamko mdogo wa wanawake kudai haki zao ikiwemo umiliki wa ardhi na mali nyinginezo.

Ø  Ushirikishwaji hafifu wa wanachi katika kupanga vipaumbele na mipango ya maendeleo ya vijiji vyao.

Ø  Ushiriki hafifu wa wanawake katika vyombo vya maamuzi.

Ø  Kuna haja ya kuwa na midahalo ya wanaume na wanawake.

Ø  Wanawake kutokuwa wawazi kwa kuuliza maswali na kutoa michango kwenye mikutano ya hadhara kutokana na mfumo dume.

Ø  Uwepo wa mila kandamizi dhidi ya wanawake katika umiliki wa ardhi na mali nyinginezo.

Ø  Elimu ya sheria ya ardhi, ndoa na milathi bado haijafahamika vizuri kwenye jamii.

MAFANIKIO.

ü  Mwitikio mkubwa wa viongozi wa vijiji na  wananchi katika kupata elimu juu ya usawa katika umiliki wa ardhi na mali nyinginezo.

ü  Ushiriki chanya wa wajumbe kutoka halmashauri (ardhi wilaya) ambao umesaidia kufikisha elimu stahiki katika jamii na njia stahiki katika utoaji na umilikishaji wa ardhi kwa wananchi na utoaji wa hati za kimila.

ü  Wananchi wamepata hamasa juu ya umiliki wa ardhi kwani wameanza kudai umiliki wa ardhi na waliokuwa wanaonewa wameanza kuripoti katika vyombo vya maamuzi vya vijiji.

ü  Viongozi wa vijiji  na kuanza kutoa elimu ya katika vijiji vyao juu ya usawa wa umiliki wa ardhi katika jamii.

ü  Mabaraza ya ardhi ya vijiji na kata yameongezewa uwezo na kuna baadhi ya mashauli ya migogoro ya ardhi yaliyoanza kushughulikiwa kwa haraka ili kuwapa haki waliowasilisha malalamiko hayo.

ü  Baada ya kupata elimu wanawake na wasichana wamehamasika juu ya umiliki wa mali na ardhi kwa kupeleka malalamiko yao kwa viongozi ili wapate haki. Washiriki walishiriki kikamilifu katika kuuliza maswali na kufanya majadiliano yaliyosaidia kuelewa kile kilichojadiliwa. Washiriki walibadilisha uzoefu juu ya njia bora za utatuzi wa migogoro.

ü  Wananchi hasa wanawake wamehamasika na wameanza kujiorodhesha kwaajili ya kupata hati miliki za kimila kwa wale ambao tayari wameshapata ardhi kwa kurithi na waliopewa na serikali za vijiji.

ü  Jamii imetambua umuhimu wa kuwa na Hati milki na kuandika wosia.

ü  Wananchi na viongozi wa vijiji wamehamasika na kuweka mpango wa ndani wa kujenga/kutenga vyumba maalumu (masijala ya ardhi) ili kuwezesha utunzwaji wa hati za wananchi katika masijala hizo.

ü  Shughuli zote zimefanyika kama zilivyopangwa.


CHANGAMOTO.

Ø  Baadhi ya vijiji kutumia fursa ya mikutano inayoitishwa na wadau kuita wajumbe wanaona wanafaa kwa kwa shughuli zao za kijiji.

Ø  Idadi kubwa wa watendaji wanaojitolea wasio na uzoefu wa kutosha katika masuala ya uongozi.

Ø  Katika mikutano ya hadhara baadhi ya wanachi kuja wakiwa wamelewa na kuleta vurugu.

Ø  Kuingiliana kwa ratiba kutokana na zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya utaifa.

Ø  Wanawake bado wanauoga wa kuzungumza/kujieleza.

Ø  Baadhi ya ya vijiji kuwa na uitikadi wa kisiasa na kupelekea ushiriki hafifu kwenye mikutano ya hadhara inayokuwa imeitishwa na wadau wa maendeleo.

Ø  Ubovu wa miundombinu ya barabara ulisababisha kuchelewa kufika katika mdahalo.

HADITHI BORA

ASANTENI KWA USIKIVU!!!!

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE