January 15, 2018

SIASA HIZI JIMBO LA IRINGA MJINI NI SIASA ZA OVYO KABISA ZISIFUMBIWE MACHO ...

kamanda  wa  polisi wa mkoa wa Iringa Julius MjengiKWA  haya  yanayoanza  kujitokeza  jimbo la Iringa mjini si  siasa  ni mwanzo  wa machafuko   kuna haja  ya  vyombo  vya ulinzi na usalama  vya  wilaya na  mkoa  kuchukua hatua za haraka siasa zisivuruge amani yetu.

Si mara  moja  ama  ni  jambo  jipya  kwa chama  chochote  cha  siasa  ama  kiongozi  wa  kisiasa aliyechaguliwa kujiuzulu  na  kujiunga na chama chochote anachokipenda na  hiyo  ndio  Demokrasia ya  vyama  vingi na  uhuru  wa  kila mmoja kuchagua  chama anachokipenda .

Ikumbukwe kabla ya  mfumo  wa  vyama  vingi  kuanza mara  nchi  baada ya  kupata  Uhuru  wake  Mwaka 1961  mwaka 1977 vyama  viwili  tawala - TANU na AFRO SHIRAZI PARTY viliungana na kuunda Chama cha Mapinduzi(CCM) na Tanzania ilirudisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi wake wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na Chama Cha Mapinduzi kilishinda na kinaendelea kutawala  hadi  leo .

Na  mfumo  huu  wa si  mgeni nchini una historia ndefu inayoanzia tangu wakati wa ukoloni. Wakati huo Tanganyika ilikuwa na vyama kama vile African National  hivyo kama  ni  mfumo  wa muda mrefu leo kwanini tuwe na  chuki  za  kisiasa kwa  wanaojiunga na  vyama  vingine maana  tunavyo vyama  zaidi ya 14  Tanzania  na CCM ndicho  chama tawala  ni  wazi  wengi  wao  wamejiunga  na  upinzani  kutoka  CCM .

Hivi leo kama chuki  hizi  za Kisiasa  zinazoaminika  kuanza  kujitokeza jimbo la Iringa mjini  zingefanywa na CCM kwa  viongozi  wake  kujiuzulu na kujiunga na upinzani  hali ya amani  ingekuwa vipi ? Iringa turejee katika  siasa  za  kweli  tusifanye  siasa  za  chuki .

 Mbunge  wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) ambae  madiwani  wake  wanajiuzulu na  amepata  kutoa  kauli  kuwa akijiuzulu  nyumba yake ichomwe  moto
USIKOSE  MAKALA  HAYA  KATIKA  GAZETI LA RAI  ALHAMISI  HII 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE