January 26, 2018

SERIKALI YASEMA UKOMA SI UGONJWA WA KULOGWA


MMG_7301
Na Florah Raphael.
Ikiwa ni miaka 64 tangu kuanzishwa kwa siku ya ukoma duniani toka mwaka 1954, Leo Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku hiyo huku kaulimbiu ikiwa ni “tokomeza ulemavu unaotokana na ukoma miongoni mwa vijana”.
Akiongea na vyombo vya habari Leo makao makuu ya Wizara ya afya kwa niaba ya waziri mkuu, naibu waziri wa afya Faustine Ndugulile amesema kuwa katika maadhimisho hayo lengo la kuikumbusha jamii na kuielimisha juu ya ugonjwa wa ukoma na kuongeza kuwa bado kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.
Akitaja maeneo ambayo bado yana changamoto ya ukoma Ndugulile amesema kuwa kuna mikoa 10 ambayo inagundua wagonjwa wapya kila mwaka ambayo ni Lindi, Rukwa, Mtwara, Morogoro, Pwani, Tanga, Geita, Dodoma, Tabora na kigoma.
Lakini pia amezitaja wilaya 20 ambazo kiwango cha ukoma kipo juu sana na bado hazijafikia lengo la utokomezaji ambazo ni Liwale, Nkasi, Ruangwa, Nanyumbu, Shinyanga manispaa, Kilombero, Mafia, Pangani, Mvomero, Masasi mjini, Lindi vijijini, Kilwa, Mpanda, Nachingwea, Rufiji, Korogwe, Mkinga, Ulanga, Morogoro vijijini na Chato.
 
Sambamba na hayo naibu waziri amezitaja dalili za awali za ugonjwa wa ukoma ambazo ni kutokwa mabaka kwenye ngozi yenye rangi ya shaba na hayawashi wala kuuma na pia mabaka haya hukosa hisia ya joto, mguso au maumivu na kuongeza kuwa dalili nyingine za ukoma ni pamoja na vijinundu kwenye ngozi hasa usoni au masikioni  na uvimbe na maumivu kwenye mifupa ya fahamu.
Pia Ndugulile ameeleza mipango ya serikali katika kutokomeza kabisa ugonjwa huo ambao hutokana na vimelea vya ukoma viitwavyo Myco-Bacteria Leprae na kusema kuwa serikali imechukua hatua ya kuendesha kampeni ya ugunduaji wa wagonjwa wapya kwa kila kijiji ndani ya harmashauli zinazoongoza hapa nchini.
Pia ameongeza  kuwa serikali imejipanga kuendesha zoezi la kutoa kinga katika ngazi ya kaya sambamba na kuagiza na kusambaza dawa za kutosha za  ukoma nchini kote.
Aidha naibu waziri  amewahasa wagonjwa wote pamoja na jamii inayowazunguka kujitokeza ili kuweza kupata matibabu yanayostahili na kuachana na mila potofu huku akisisitiza kuwa ugonjwa wa ukoma siyo ugonjwa wa kurogwa na kuongeza kuwa matibabu ya ukoma hutolewa bure kabisa katika vituo vyote vya afya hapa nchini.
 
Mwisho kabisa naibu waziri ameiomba jamii kujenga tabia ya kuchunguza miili yao Mara kwa Mara ili kuweza kuuzuia ugonjwa ukiwa katika hatua ya awali jambo ambalo litasaidia pia kupunguza kusambaa kwa ugonjwa huo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE