January 22, 2018

SERIKALI KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA KUNUFAIKA NA BOMBA LA HOIMA


P1
Kamishna Msaidizi wa Mafuta toka Wizara ya Nishati Bibi. Mwanaamani Kidaya akimwelekeza jambo Mratibu wa Mradi wa Bomba la Mafuta toka Hoima , Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania wakati wa mkutano wa wadau wa Mafuta toka sehemu mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.
P2
Mwakilishi wa Kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa Mafuta, Gulf Interstate Engineering akiwasilisha mada kuhusu fursa na vigezo vitakavyotumika kutoa ajira wakati wa ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta toka Hoima , Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania wakati wa mkutano wa wadau wa Mafuta toka sehemu mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.
P3
Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATGOS), Abdulsamad Abdulrahim akielezea namna ambavyo wazawa wanaweza kunufaika na ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Hoima , Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania wakati wa mkutano wa wadau wa Mafuta toka sehemu mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.
P4a
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wadau kutoka sekta binafsi na makampuni mbalimbali ya kimataifa kujadili ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
P4b
P4c
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wadau kutoka sekta binafsi na makampuni mbalimbali ya kimataifa kujadili ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.Picha na: Frank Shija – MAELEZO
………………………………………………………………………………………….
Na: Mwandishi Wetu-MAELEZO-DAR ES SALAAM
 SERIKALI imesema itasimamia maslahi ya Wajasiriamali na makampuni ya Kitanzania yatayokidhi viwango vya kimataifa katika utoaji wa huduma ili kuwaweka kunufaika na fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kaabale nchini Uganda hadi ghuba ya Chongoleani Tanzania.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Mafuta katika Wizara ya Nishati, Mwanaamani Kidaya wakati wa warsha iliyoandaliwa na iliyoshirikisha Wadau kutoka sekta binafsi na makampuni mbalimbali ya kimataifa kujadili ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
Bi. Mwanaamani alisema ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania ni fursa ya kipekee ambayo haina budi kutumiwa kikamilifu kwa ajili ya kuinua uchumi wa Tanzania, hivyo ni wajibu wa makampuni na wajasiriamali kuhakikisha kuwa wanatimiza viwango katika vifaa vitakavyokuwa vikihitajika na makampuni za ukandarasi zitakazokuwa zikisimamia ujenzi huo.
“Mradi huu unatarajia kupita katika mikoa 8 ya Tanzania, ambapo kati ya kilometa 1445 za bomba hilo, kilometa 1147 zipo Tanzania, hivyo ni wajibu wa makampuni yetu kuhakikisha kuwa zinakidhi viwango vya kimaitafa vinavyowekwa na makampuni ya ukandarasi na Serikali itawasimamia” alisema Mwanaamini.
Aidha Mwanaamini alisema mradi huo wa bomba la mafuta unatarajia kutekelezwa katika viwango vya kimataifa, ambapo huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinatarajia kuwanufaisha wananchi wa mataifa ya Tanzania na Uganda, hivyo makampuni ya Kitanzania hayana budi kuhakikisha kuwa yanatoa huduma bora zinazoendana na viwango vya hali juu.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATGOS), Abdulsamad Abdulrahim alisema warsha hiyo imeshirikisha watalaamu kutoka Mataifa mbalimbali duniani ili kuwawezesha Watanzania kuelewa viwango vya kimataifa vinavyotumika kwa ajili ya kujenga miradi mbalimbali ikiwemo bomba la mafuta.
Aliongeza kuwa kongamano hilo pia ni limelenga pia kujenga uwezo na fursa makampuni na wajasiriamali wa Watanzania kupata uelewa kuhusu utekelezaji wa mradi wa bomba la gesi pamoja na fursa mbalimbali wanazopaswa kuzitumia ili ziweze kuwainua kiuchumi.
“Makampuni kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Uingereza, Kuwait, Dubai, India, Malaysia, Argentina na Marekani yameshiriki katika mkutano huu, hivyo ni wajibu wa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo katika bomba la mafuta ambalo litaweza kuzalisha ajira kwa wananchi wengi zaidi” alisema Abdulrahim.
Abdulrahim alisema kuwa kwa sasa ujenzi wa bomba hilo umefikia katika hatua nzuri ya utekelezaji wake, na kuwataka Watanzania kuwa tayari wakati mchakato wa kutafuta kampuni mbalimbali za ukandarasi utakapoanza kutangazwa na Serikali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye alisema mradi wa ujenzi wa bomba hilo unatarajia kuzalisha ajira nyingi kwa Watanzania, hivyo ni wajibu wa makampuni ya Kitanzania kuhakikisha kuwa yanafanya kazi kwa kuzingatia viwango na maadili ya kimataifa.
Aliongeza kuwa TPSF itahakikisha kuwa inaisimamia Serikali katika kutoa taarifa za mapema na haraka zaidi kwa Watanzania kupitia zabuni zitakazotangazwa na makampuni mbalimbali pindi mchakato wa ujenzi wa bomba hilo utakapoanza.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE