January 30, 2018

RC MASENZA ATAKA MAHAKAMA KUTUMIA TEHAMA KUTENDA HAKI

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina  Masenza (katikati)  akiongoza maandamano ya uzinduzi wa  wiki ya sharia nchini nyuma ni mstahiki  meya  wa Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe na  mbele kushoto  ni jaji mfawidhi Iringa Mary Shangali  na mkuu  wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  kulia
Maandamano ya  uzinduzi wa  wiki ya  sharia 
Wananchi  mbali mbali na  vyombo  vya  ulinzi  wakiwa katika maandamano ya uzinduzi wa  wiki ya  sharia nchini kwa  mkoa  wa Iringa
Baadhi ya  mawakili walioshiriki maandamano hayo
 

Picha na habari  na matukiodaimaBlog
MKUU  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama Pamoja na mahakama kutenda haki kwa kutumia tehama .
 
“Niwaombe kila mmoja kwa nafasi yake kupitia tehama  tutimize wajibu wetu kurahisisha utoaji wa haki kwa wakati kwa kuheshimu sharia, kanuni na taratibu; kwa kuzingatia muda uliowekwa kisheria kwa kila hatua ya shauri kufanyika” alisema mkuu huyo wa mkoa
 
Akizungumza  katika uzinduzi  wa wiki ya sheria jana katika  viwanja  vya mahakama kuu kanda ya Iringa mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa TEHAMA itumike kutunza kumbukumbu vizuri, upelelezi, mawasiliano, uratibu na majumuisho wakati wa utoaji haki.
 
Alisema kuwa maudhui ya Wiki ya Sheria mwaka huu ni “matumizi ya Tehama katika utoaji haki kwa wakati na kwa kuzingatia maadili
 
Hivyo dhana ya huduma ya haki kuwa Katiba  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Ibara 107 A (2) (d) na (e) inatamka bayana kuwa Mahakama katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia Sheria, na zitafuata kanuni .
 
Alizitaja kanuni hizo kuwa  Kutochelewesha haki na Kutenda haki.
 
“Hivyo Katiba na Sheria zetu nchini zinatambua umuhimu wa huduma ya haki kwa mwananchi lakini ili iwe yenye tija lazima haki hiyo itolewe kwa wakati’’
 
Masenza alisemakuwa pamoja na miongozo ya kisheria iliyopo, bado tumeshuhudia changamoto za utoaji haki katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, ikicheleweshwa,  ikiwa ni pamoja na mlundikano wa wahalifu, mahabusu, mashauri kutoisha kwa wakati .
 
“kwa visingizio mbalimbali, ucheleweshaji wa utoaji haki na wakati mwingine hata haki yenyewe kuto patikana kabisa”
 
Alisema kuwa gharama kubwa za uendeshaji mashauri na usumbufu wa utoaji ushahidi na  mambo ambayo yanapaswa kukomeshwa .
Hata  hivyo alisema ukiliangalia jambo hili, ni mtambuka na kwa sababu hiyo ni muhimu kila muhusika asiwe chanzo cha kuchelewesha upatikanaji wa haki. 
 
 
Kwani alisema      Tehama inasaidia kutunza kumbukumbu zote muhimu za mwenendo wa kesi na mwisho wa siku haki kutolewa kwa wakati.
 
“TEHAMA inasaidia kuwaondolea wadau usumbufu na gharama za kuhudhuria mahakamani mara kwa mara na kwa muda mrefu”
 
Kwa  upande  wake jaji mfawidhi  wa Iringa Mary Shangali  alisema  kuwa katika utekelezaji wa mpango mkakati wa  miaka mitano wa mahakama kurugenzi ya Tehama imepewa majukumu  ya kuboresha  huduma za  kimahakama na  kuhakikisha  uwepo  wa miundo mbinu sahihi.
 
“ Mfumo  wa  kuratibu nyaraka  KI-eletronic na  huduma  za kimahakama  kwa  njia ya  mtandao  haya yote tutayazungumza vizuri  siku ya  sheria nchini  tutawaeleza hatua  tulizochukua”

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE