January 17, 2018

Papa akabiliwa na shinikizo kuhusu ukiukaji wa kingono Chile

Image result for Papa chile
Kiongozi wa Kanisa katoliki Duaniani Papa Francis atakuwa chini ya shinikizo leo kukabiliana na kashfa ya Padri mmoja inayohusu unyanyasaji wa kingono wakati wa siku yake ya kwanza nchini Chile, taifa ambalo wengi wa raia wake ni wafuasi wa madhehebu ya Kikatoliki, lakini ambako wasiwasi na hata dharau miongoni mwa waumini hao umekuwa ukizidi dhidi ya kanisa Katoliki. 
Raia wengi wa Chile bado wana ghadhabu juu ya uamuzi wake wa kumteua askofu ambaye ni mtu wa karibu na Mchungaji Fernando Karadima, padri aliyekutikana na hatia na Vatican mwaka 2011 ya kuwanyanyasa kijinsia watoto kadhaa wa umri mdogo kwa kipindi cha muongo mzima. 
Askofu Juan Barros kutoka mji wa kusini wa Osorno amekanusha kwamba alikuwa akijua alichokuwa akikifanya Karadima lakini raia wengi wa Chile hawamuamini. 
Kupotea kwa uaminifu huo kunamuathiri pia Francis ambaye anafanya ziara yake ya kwanza kama papa katika taifa hilo la watu milioni 17.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE