January 15, 2018

NYUMBA YA DIWANI ALIYEJIUZULU CHADEMA YAHUJUMIWA YAVUNJWA NA WATU WASIOJULIKANA


ZIKIWA zimepita siku takribani 9 toka aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwangata Jimbo la Iringa mjini Anjelius Lijuju (chadema)kujiuzulu nafasi yake watu wasiojulikana wameivunja Nyumba yake aliyokuwa akijenga.

Akizungumza na Mtandao  wa matukiodaima,Lijuju alisema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana  .

"Nilipata taarifa toka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa kuwa Nyumba yangu imevamiwa usiku na kubomolewa na mtu ama watu wasiojulikana"

Alisema baada ya taarifa hiyo alifika kuona kabla ya kuripoti polisi ambao walifika eneo la tukio.

Lijuju amelihusisha tukio hilo na chuki za kisiasa ambazo zimekuja baada ya yeye kujiuzulu nafasi yake ya udiwani kwa kile alichodai ni kutokana na udiktate wa viongozi wa chama hicho.

"Kama kweli siasa zinatufikisha hapa nchi hii inakokwenda siko Mimi kuhama kwangu na kuvunjiwa Nyumba kuna mahusiano gani "

Hivyo aliomba vyombo vya dola kufanya kazi yake ili wahusika wajulikane na kuchukuliwa hatua.

Kwani alisema alikuwepo ndani ya chama hicho na anajua kazi inayofanywa na vikosi vya ulinzi ndani ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kutumwa na viongozi kupambana na wale wanaokwenda kinyume na chama hicho.

Alisema kuwa mbunge Mchungaji Peter Msigwa akiwa katika mkutano wake Mlandege alitaka wananchi kuvunja Nyumba yake iwapo atahama chama kauli aliyoitafsiri kuwa ndio inafanya kazi.

Hata hivyo alisema alikuwa bado hajaamua kujivua uanachama wa chama hicho ila sasa atatangaza kujivua na kuhamia kabisa CCM.


Mke wa Diwani Hugo aliyejiuzulu chadema Christina Lijuju alisema kuwa ameumizwa sana na Nyumba hiyo kuvunjwa kwani wameanza kujenga zaidi ya miaka mitano sasa bila kukamilika.

"Ninaomba sana serikali ya Rais Dkt John Magufuli itusaidie kuwasaka watu hao wasiojulikana waliovunja Nyumba yetu"

Kuwa iwapo watu hao wasiojulikana wakaendelea kufanya uharifu nchi haitakalika kwani inaumiza sana.

Huku Diwani wa Kata ya Ndiuka Mussa Mlawa ( chadema) kuwa amesikitishwa sana na kitendo hicho na kuwa kuanzia sasa wanaanzisha ulinzi wa sungusungu .

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa Julius Mjengi hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE