![]() |
Nape akibadilishana mawazo na Dk. Ndumbaro |
MBUNGE
wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi Nape Nnauye amefunguka kwa kudai kuwa
hawezi kukihama chama cha mapinduzi (CCM) kama baadhi ya watu wakiwemo
wa vyama vya upinzani kwa kile alichodai kuwa magari ya upinzani
yanaenda kuzama na hayajulikani yataibuka lini.
Uwazi
huo ameuweka jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Songea
mjini mkoani Ruvuma kwa tiketi ya CCM Dk, Damas Ndumbaro kwenye mkutano
wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya bombambili Manispaa ya Songea.
Nnauye
ambaye aliwahi kuwa katibu wa hitikadi na uenezi CCM taifa na Waziri wa
Habari, Michezo na Sanaa katika serikali ya awamu ya tano alisema kuwa
kama kuna watu walidhani atakihama chama cha mapinduzi (CCM) na kwenda
upinzani wasahau kabisa .
Akizungumza
kwa kujiamini huku akishangiliwa na mamia ya wakazi wa bombambili
alisema kuwa kama kuna kuwa na matatizo ndani ya CCM tunaonyana ndani ya
chama na kuyamaliza na siyo kuhama chama.
“Naikubali
serikali ya awamu ya tano inayongonzwa na jemedali Dk. John Magufuli
pamoja na makamu wa Rais na waziri mkuu wake kuwa ipo imara na mimi
naapa kufia CCM na siyo vinginevyo” alisema Nape Nnauye.
“Nasikia
maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia
upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na
mawazo hayo” alisema mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
Katika
kampeni hizo ambazo uchaguzi wake utafanyika Januari 13 mwaka huu Nape
Nnauye na Moses Machali aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kasulu mkoa wa
Kigoma kwa tiketi ya NCCR Mageuzi wamekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi
wa jimbo la Songea hasa wanapokuwa majukwani.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE