January 16, 2018

Mwizi aliyevalia kama mtawa aiba $35,000 nchini Kenya

Mwizi huyo alivalia kama mtawa na kuibia duka la kubadilishana sarafu Kenya
Maafisa wa polisi nchini Kenya wameanzisha msako dhidi ya mwanamke aliyevalia kama mtawa na kufanikiwa kuibia duka la kubadilisha sarafu takriban dola 35,000.
Kasi ya wizi huo imewashangaza wachunguzi.
Duru karibu na wachunguzi zimeilezea BBC kuwa mwanamke huyo aliyevalia kama mtawa aliingia katika duka la kubadilishia sarafu kabla ya muhudumu kumpa pesa za sarafu 15 mbalimbali.
Picha za kamera za CCTV kutoka kwenye duka hilo zinamwonyesha mwanamke huyo akielekea hadi kwenye sehemu ya kuhudumiwa kama mteja baada ya kukaguliwa kwenye mlango.
Kisha anazungumza na muhudumu kabla ya kukubaliwa kuingia eneo ambalo pesa huwekwa kupitia mlango salama wa chuma.
Baada ya muda kidogo wa mazungumzo, muhudumu anamfungulia kasha la chuma ambapo pesa zilikuwa kabla ya kuanguka kwenye kiti.
Wizi wote ulichukua chini ya dakika kumi na mlinzi wa langoni hakugundua kilichokuwa kikiendelea.
Wachunguzi wanashuku kulikuwa na ushirikiano kutoka kwa wafanyikazi wa duka hilo na tayari wamemkamata mhudumu aliyehusika.
Mwezi Novemba mwaka jana, wezi walichimba handaki lenya urefu wa mita thelathini na kuiba dola alfu mia tano kutoka kwa benki moja mjini Thika, kilomita 40 Kaskazini Mashariki mwa Nairobi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE