January 19, 2018

MWENYEKITI BAVICHA IRINGA MJINI AKAMATWA NA POLISI ,MBUNGE MSIGWA NA MEYA WATAKIWAKUJISALIMISHA

Mwenyekiti wa BAVICHA Iringa mjini Bw  Marto

JESHI  la polisi  mkoa  wa  Iringa   linamshikilia  mwenyekiti  wa baraza la  vijana  wa  chama  cha  Demokrasia na  Maendeleo (CHADEMA)  wilaya ya  Iringa  mjini Leonce Marto kwa  tuhuma  za  kuhusika na tukio la  kuvunjiwa  nyumba  diwani  wa kata ya Mwangata Angelus Lijuja aliyehama chama  cha Chadema.

Akizungumza na  mtandao  huu  wa matukiodaima  ofisini kwani kaimu kamanda wa mkoa  wa  Iringa John Kauga  alisema  kuwa  Marto amekamatwa  toka juzi  na  kuwa  msako wa kusawaka wengine  waliohusika unaendelea na  baadhi yao  wamekamatwa .

Bila  kutaja  majina  ya  wanaotafutwa  na jeshi la  polisi  kuhusika na matukio ya uvunjaji wa   nyumba  na uchomaji  moto  wa  nyumba aliyokuwa amepanga katibu  wa  umoja wa  vijana   wilaya ya  Iringa mjini Alphonce Muyinga  ,Kauga  alisema  kuwa  wameanza msako mkali  kuwatafuta  na  kuwakamata  wote  waliohusika.

"  Ninachotaka  kusema  jeshi la  polisi   si  jeshi la  kurumbana na mtu  kwenye  mitandao ya kijamii  tunafanya kazi  yetu kwa  kuzingatia  weledi hivyo kauli za  mbunge wa jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa  kututaka  kuacha kukamata watuhumiwa na matukio hayo si ya  msingi hili  si jeshi la kuagizwa na mbunge "

Alisema   kuwa  kuna  orodha  ndefu ambayo  imetangazwa na viongozi wa BAVICHA mkoa  kuwa  wanatafutwa na  polisi  hiyo ni orodha  yao sio ya  jeshi la  polisi  sisi  tunaowatafuta  orodha  yetu  ni  siri  yetu   ila kama mbunge Mchungaji Msigwa  na meya  wa  Iringa mjini Alex Kimbe  wanajua kama  wanatafutwa  basi  wajisalimishe polisi  wenyewe .

Kwani  alisema kwa  yeyote  ambaye anatafutwa na  jeshi la  polisi kwa  matukio hayo ya  uvunjifu wa amani  mjini Iringa atasakwa  popote  alipo hata  iwe  chini ya  uvungu hawatamuacha hata  mmoja .

Kauga  alisema  kuwa sababu ya kukamatwa  kwa Marto  ni kutokana na kauli ya  kichochezi wlizozitoa  pamoja na  mbunge kwenye mkutano  wao uliofanyika  Mlandege mjini hapa  hivi karibuni   kuwa nyumba  ya mbunge Msigwa akijiuzulu  chadema  ichomwe  moto  .

Kuwa  baada ya  kauli  hiyo wananchi  walihoji  kuwa na madiwani  wanaojiuzulu  chadema  nyumba  zao zifanyweje  mbunge Msigwa  alisema  muda  umekwisha  ila  ujumbe umefika .
Hata  hivyo  Kauga  alisema  kuwa baadhi ya viongozi  wa Chadema mkoa  na  wilaya  pamoja na naibu meya  wa Manispaa ya  Iringa Dady  Igogo wamehojiwa na kuachiwa huru  jana .

Kwa  upande  wake katibu wa BAVICHA  mkoa  wa Iringa Jackson  Mnyawami  akizungumza na  vyombo  vya habari  juu ya  kukamatwa  kwa  viongozi  wa  Chadema alisema  kuwa  miongoni mwa  viongozi  wanatafutwa ni pamoja  na  mbunge Mchungaji Msigwa , Meya   Kimbe  na  wengine .

Hivyo  alitaka  jeshi la  polisi  kutenda haki katika  kamata  kamata  inayoendelea na  kuwa  Chadema wanalaani  matukio ya  uvunjaji wa amani katika Manispaa ya  Iringa kwani wao si  wahusika  wa   tukio la kuvunjiwa  nyumba  Diwani Lijuja  aliyehama Chadema na katibu  wa  UVCCM wilaya ya  Iringa mjini.

Pia  alikitaka  chama  cha  CCM kuacha  jeshi la  polisi kufanya kazi yake  bila  kuwaingilia na  kuwaonyesha  nani na nani  wakamatwe katika matukio  hayo .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE