January 12, 2018

MREMA ATINGA POLISI NI KUHUSU WATANZANIA HAWA.....

 

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema leo Ijumaa ametoa taarifa za kuzushiwa kifo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay wilayani Kinondoni ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Juzi katika mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za kufariki kwa mwanasiasa huyo lakini muda mfupi baadaye Mrema alikanusha akisema ni mzima wa afya njema.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Mrema amesema yupo Oysterbay kutoa taarifa ili suala hilo lichunguzwe na Jeshi la Polisi ili wamnase aliyesambaza taarifa hizo.
“Nipo Oysterbay Polisi namalizia taratibu za kuandikisha kesi hii, nikimaliza nitakujulisha kwa kina kuhusu suala hili,” amesema.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE